Romans 9:4 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hao ndio watu wa Israeli ambao Mungu aliwateua wawe watoto wake, akawashirikisha utukufu wake; alifanya nao maagano, akawapa sheria yake, imani ya kweli na ahadi zake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
yaani watu wa Israeli. Hao ndio wenye kule kufanywa wana, ule utukufu wa Mungu, yale maagano, kule kupokea Torati, ibada ya kwenye Hekalu na zile ahadi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
ambao ni Waisraeli, wenye kule kufanywa wana, na ule utukufu, na maagano, na kupewa torati, na ibada ya Mungu, na ahadi zake;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ni Waisraeli, watoto waliochaguliwa na Mungu. Wameushuhudia utukufu wa Mungu na wanashiriki maagano aliyofanya Mungu na watu wake. Mungu aliwapa Sheria ya Musa, ibada ya Hekalu, na ahadi zake.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hao ndio watu wa Israeli ambao Mungu aliwateua wawe watoto wake, akawashirikisha utukufu wake; aliagana nao, akawapa Sheria yake, imani ya kweli na ahadi zake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hao ndio watu wa Israeli ambao Mungu aliwateua wawe watoto wake, akawashirikisha utukufu wake; alifanya nao maagano, akawapa sheria yake, imani ya kweli na ahadi zake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
yaani, watu wa Israeli, ambao ndio wenye kule kufanywa wana, ule utukufu wa Mungu, yale maagano, kule kupokea sheria, ibada ya kwenye Hekalu na zile ahadi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
yaani, watu wa Israeli, ambao ndio wenye kule kufanywa wana, ule utukufu wa Mungu, yale maagano, kule kupokea sheria, ibada ya kwenye Hekalu na zile ahadi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
ambao ni Waisraeli, wenye kule kufanywa wana, na ule utukufu, na maagano, na kupewa torati, na ibada ya Mungu, na ahadi zake;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hao ndio watu wa Israeli ambao Mungu aliwateua wawe watoto wake, akawashirikisha utukufu wake; alifanya nao maagano, akawapa sheria yake, imani ya kweli na ahadi zake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kweli ndio Waisiraeli, tena ni wana, hata utukufu wanao, walipewa maagano na maonyo na tambiko lililo la kweli na viagio.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
ambao ni Waisraeli, wenye kule kufanywa wana, na ule utukufu, na maagano, na kupewa torati, na ibada ya Mungu, na ahadi zake;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
ndilo taifa la Waisraeli. Wao walikubaliwa na Mungu kuwa watoto wake, yeye aliwaonyesha utukufu, alifanya maagano nao, aliwapa Sheria, aliwaonyesha namna ya kumwabudu na kuwatolea ahadi zake.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
ambao ni Waisraeli, wenye kufanywa wana, wenye utukufu na maagano, wenye kupewa torati na ibada ya Mungu na ahadi zake; ambao mababu ni wao,