Romans 9:7 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wala si wazawa wote wa Abrahamu ni watoto wake wa kweli. Ila, kama yasemavyo Maandiko Matakatifu: “Wazawa wake watatokana na Isaka.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wala hawawi wazao wa Ibrahimu kwa sababu wao ni watoto wake, lakini: “Uzao wako utahesabiwa kupitia kwake Isaka.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wala hawawi wote wana kwa kuwa wazao wa Ibrahimu, bali, Katika Isaka wazao wako wataitwa;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Na hivyo ni baadhi tu ya watoto wa Ibrahimu ndiyo wazaliwa wake halisi. Hivi ndivyo Mungu alimwambia Ibrahimu: “Wazaliwa wako halisi watakuwa wale waliotoka kwa Isaka.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Wala, si wazawa wote wa Abrahamu ni watoto wake wa kweli. Ila, kama yasemavyo Maandiko Matakatifu: “Wazao wake watatokana na Isaka.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wala si wazawa wote wa Abrahamu ni watoto wake wa kweli. Ila, kama yasemavyo Maandiko Matakatifu: “Wazawa wake watatokana na Isaka.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wala si tu kwamba kwa sababu wamezaliwa na wazao wa Abrahamu ni watoto wake, lakini ahadi ya Mungu kwa Abrahamu ilikuwa: “Watoto wako watahesabiwa katika uzao wa Isaki.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wala hawakuwi wazao wa Ibrahimu kwa sababu wao ni watoto wake, lakini: “Uzao wako utahesabiwa kupitia kwake Isaka.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wala hawawi wote wana kwa kuwa wazawa wa Abrahamu, bali, Katika Isaka wazawa wako wataitwa;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wala si wazawa wote wa Abrahamu ni watoto wake wa kweli. Ila, kama yasemavyo Maandiko Matakatifu: “Wazawa wake watatokana na Isaka.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wala walio wa uzao wake Aburahamu sio wote hata watoto. Ila imeandikwa: Watakaoitwa uzao wako ni wa Isaka tu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wala hawawi wote wana kwa kuwa wazao wa Ibrahimu, bali, Katika Isaka wazao wako wataitwa;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
wala si wote wanaotoka katika uzao wa Abrahamu, ndio watoto wa kweli wa Abrahamu. Kwa kuwa Mungu alimwahidia Abrahamu: “Ni kwa njia ya Isaka utapata wazao watakaoitwa wako.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Wala hawawi wote wana kwa kuwa wazao wa Ibrahimu, bali, Katika Isaak wazao wako watakwitwa;