Romans 9:8 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ndiyo kusema, si wale waliozaliwa kimaumbile ndio watoto wa Mungu, bali wale waliozaliwa kutokana na ahadi ya Mungu ndio watakaoitwa watoto wake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hii ina maana kwamba, si watoto waliozaliwa kimwili walio watoto wa Mungu, bali ni watoto wa ahadi wanaohesabiwa kuwa uzao wa Ibrahimu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
yaani, si watoto wa mwili walio watoto wa Mungu, bali watoto wa ile ahadi wanahesabiwa kuwa wazao.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hii ina maana kuwa si watoto wote wa Ibrahimu walio watoto halisi wa Mungu. Wazaliwa halisi wa Ibrahamu ni wale wanaofanyika watoto wa Mungu kwa sababu ya agano ambalo Mungu alililiweka na Ibrahamu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Nido kusema, wale waliozaliwa kimaumbile ndio watoto wa Mungu, bali wale waliozaliwa kutokana na ahadi ya Mungu ndio watakaoitwa watoto wake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ndiyo kusema, si wale waliozaliwa kimaumbile ndio watoto wa Mungu, bali wale waliozaliwa kutokana na ahadi ya Mungu ndio watakaoitwa watoto wake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hii ina maana kwamba, si watoto waliozaliwa kimwili walio watoto wa Mungu, bali ni watoto wa ahadi wanaohesabiwa kuwa uzao wa Abrahamu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hii ina maana kwamba, si watoto waliozaliwa kimwili walio watoto wa Mungu, bali ni watoto wa ahadi wanaohesabiwa kuwa uzao wa Ibrahimu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
yaani, si watoto wa mwili walio watoto wa Mungu, bali watoto wa ile ahadi wanahesabiwa kuwa wazawa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ndiyo kusema, si wale waliozaliwa kimaumbile ndio watoto wa Mungu, bali wale waliozaliwa kutokana na ahadi ya Mungu ndio watakaoitwa watoto wake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ni kwamba: Walio watoto wa kimtu hao sio watoto wake Mungu; ila walio watoto wa kiagio huwaziwa kuwa uzao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
yaani, si watoto wa mwili walio watoto wa Mungu, bali watoto wa ile ahadi wanahesabiwa kuwa wazao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Maana yake, si wale waliozaliwa sawa na kawaida wanaohesabiwa kuwa watoto wa Mungu; lakini ni wale waliozaliwa kufuatana na ahadi ya Mungu ndio wanaohesabiwa kuwa wazao wake wa kweli.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
yaani, si watoto wa mwili walio watoto wa Mungu, bali watoto wa ile ahadi wanabesabiwa kuwa wazao.