Ruth 1:19 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ndipo wote wawili wakaendelea na safari hadi Bethlehemu. Walipofika huko, watu wote walishangaa, hata wanawake wakaulizana, “Je, huyu ni Naomi?”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo hao wanawake wawili wakaondoka, wakafika Bethlehemu. Walipofika Bethlehemu, mji mzima ulitaharuki, wanawake wakashangaa, wakasema, “Huyu aweza kuwa ni Naomi?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hivyo hao wakaendelea wote wawili hata walipofika Bethlehemu. Na ikawa walipofika Bethlehemu, mji wote ulitaharuki kwa habari zao. Nao wanawake wakasema, Je! Huyu ni Naomi?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ndipo wote wawili wakaendelea na safari hadi Bethlehemu. Walipofika huko, watu wote walishangaa, hata wanawake wakaulizana, “Je, huyu ni Naomi?”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo hao wanawake wawili wakaondoka, wakafika Bethlehemu. Walipofika Bethlehemu, mji mzima ulitaharuki, wanawake wakashangaa, wakasema, “Huyu aweza kuwa ni Naomi?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo hao wanawake wawili wakaondoka, wakafika Bethlehemu. Walipofika Bethlehemu, mji mzima ulitaharuki, wanawake wakashangaa, wakasema, “Huyu aweza kuwa ni Naomi?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hivyo hao wakaendelea wote wawili hadi walipofika Bethlehemu. Na ikawa walipofika Bethlehemu, mji wote uliwastaajabia. Nao wanawake wakasema, Je! Huyu ni Naomi?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ndipo wote wawili wakaendelea na safari hadi Bethlehemu. Walipofika huko, watu wote walishangaa, hata wanawake wakaulizana, “Je, huyu ni Naomi?”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakaenda wao wawili, mpaka wakifika Beti-Lehemu. Ikawa, walipofika Beti-Lehemu, mji wote ukavurugika kwa ajili yao wakisema: Kumbe huyu siye Naomi?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hivyo hao wakaendelea wote wawili hata walipofika Bethlehemu. Na ikawa walipofika Bethlehemu, mji wote ulitaharuki kwa habari zao. Nao wanawake wakasema, Je! Huyu ni Naomi?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu wote wawili wakaendelea na safari mpaka Betelehemu. Walipofika kule, watu wote wakashangaa, hata wanawake wakaulizana: “Huyu ni Naomi?”