Ruth 1:21 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nilipoondoka hapa, nilikuwa na vitu vingi, lakini sasa Mwenyezi-Mungu amenirudisha mikono mitupu. Mbona mwaniita Naomi na hali Mwenyezi-Mungu ameniadhibu, naye Mungu Mwenye Nguvu amenitesa.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mimi niliondoka hali nimejaa, lakini Mwenyezi Mungu amenirudisha mtupu. Kwa nini kuniita Naomi? Mwenyezi Mungu amenitendea mambo machungu; Mwenyezi ameniletea msiba.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mimi nalitoka hali nimejaa, naye Bwana amenirudisha sina kitu, kwani kuniita Naomi, ikiwa Bwana ameshuhudia juu yangu, na Mwenyezi Mungu amenitesa?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nilipoondoka hapa, nilikuwa na vitu vingi, lakini sasa Mwenyezi-Mungu amenirudisha mikono mitupu. Mbona mwaniita Naomi na hali Mwenyezi-Mungu ameniadhibu, naye Mungu Mwenye Nguvu amenitesa.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mimi niliondoka hali nimejaa, lakini BWANA amenirudisha mtupu. Kwa nini kuniita Naomi? BWANA amenitendea mambo machungu; Mwenyezi ameniletea msiba.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mimi niliondoka hali nimejaa, lakini bwana amenirudisha mtupu. Kwa nini kuniita Naomi? bwana amenitendea mambo machungu; Mwenyezi ameniletea msiba.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mimi nilitoka nikiwa nimejaa, naye BWANA amenirudisha sina kitu, kwani kuniita Naomi, ikiwa BWANA ameshuhudia juu yangu, na Mwenyezi Mungu amenitesa?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nilipoondoka hapa, nilikuwa na vitu vingi, lakini sasa Mwenyezi-Mungu amenirudisha mikono mitupu. Mbona mwaniita Naomi na hali Mwenyezi-Mungu ameniadhibu, naye Mungu Mwenye Nguvu amenitesa.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nilipokwenda nilikuwa mwenye mali, lakini Bwana amenirudisha mikono mitupu. Mbona mnaniita Naomi? Naye Bwana ametoa ushuhuda wa kunishinda, yeye Mwenyezi ameniumiza vibaya.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mimi nalitoka hali nimejaa, naye BWANA amenirudisha sina kitu, kwani kuniita Naomi, ikiwa BWANA ameshuhudia juu yangu, na Mwenyezi Mungu amenitesa?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nilipoondoka hapa, nilikuwa na vitu vingi, lakini sasa Yawe amenirudisha mikono mitupu. Mbona munaniita Naomi ijapokuwa Yawe ameniazibu, naye Mungu Mwenye Nguvu amenitesa?”