Ruth 1:6 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Baadaye, Naomi alipata habari kwamba Mwenyezi-Mungu alikuwa amewabariki watu wake kwa kuwapa chakula. Basi, akaondoka kutoka Moabu kurudi kwao pamoja na wakwe zake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Aliposikia akiwa huko Moabu kwamba Mwenyezi Mungu amewasaidia watu wake kwa kuwapa chakula, Naomi na wakwe wake wakajiandaa kurudi nyumbani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo alipoondoka, yeye na wakweze, ili kurudi kutoka nchi ya Moabu; maana huko katika nchi ya Moabu amesikia ya kwamba Bwana amewajilia watu wake na kuwapa chakula.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Baadaye, Naomi alipata habari kwamba Mwenyezi-Mungu alikuwa amewabariki watu wake kwa kuwapa chakula. Basi, akaondoka kutoka Moabu kurudi kwao pamoja na wakwe zake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Aliposikia akiwa huko Moabu kwamba BWANA amewasaidia watu wake kwa kuwapa chakula, Naomi na wakweze wakajiandaa kurudi nyumbani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Aliposikia akiwa huko Moabu kwamba bwana amewasaidia watu wake kwa kuwapa chakula, Naomi na wakweze wakajiandaa kurudi nyumbani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo alipoondoka, yeye na wakweze, ili kurudi kutoka nchi ya Moabu; maana akiwa katika nchi ya Moabu alipata habari kuwa BWANA alikuwa amewajia watu wake na kuwapa chakula.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Baadaye, Naomi alipata habari kwamba Mwenyezi-Mungu alikuwa amewabariki watu wake kwa kuwapa chakula. Basi, akaondoka kutoka Moabu kurudi kwao pamoja na wakwe zake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha akaondoka yeye na wakwewe, atoke kwenye mbuga za Moabu kurudi kwao, kwani alisikia kule kwenye mbuga za Moabu, ya kuwa Bwana amewakagua walio ukoo wake na kuwapa vyakula.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo alipoondoka, yeye na wakweze, ili kurudi kutoka nchi ya Moabu; maana huko katika nchi ya Moabu amesikia ya kwamba BWANA amewajilia watu wake na kuwapa chakula.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha, Naomi akapata habari kwamba Yawe alikuwa amewabariki watu wake kwa kuwapa chakula. Basi, akaondoka kutoka Moabu kurudi kwao, pamoja na wakwe zake.