Ruth 1:8 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Naye Naomi akawaambia hao wakwe zake wawili, “Rudini kila mmoja nyumbani kwa mama yake. Naomba Mwenyezi-Mungu awe mwema kwenu kama mlivyokuwa wema kwangu na kwa wale watu wangu waliofariki.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo Naomi akawaambia wale wakwe wake wawili, “Rudini, kila mmoja wenu nyumbani mwa mama yake. Mwenyezi Mungu na awatendee mema kama mlivyowatendea hao waliofariki, na mimi pia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha Naomi akawaambia wakweze wawili, Nendeni sasa mkarejee kila mmoja nyumbani kwa mamaye; Bwana na awatendee mema ninyi, kama ninyi mlivyowatendea mema hao waliofariki na mimi pia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Naye Naomi akawaambia hao wakwe zake wawili, “Rudini kila mmoja nyumbani kwa mama yake. Naomba Mwenyezi-Mungu awe mwema kwenu kama mlivyokuwa wema kwangu na kwa wale watu wangu waliofariki.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo Naomi akawaambia wale wakwe zake wawili, “Rudini, kila mmoja wenu nyumbani kwa mama yake. BWANA na awatendee fadhili kama mlivyowatendea hao waliofariki pamoja na mimi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo Naomi akawaambia wale wakwe zake wawili, “Rudini, kila mmoja wenu nyumbani kwa mama yake. bwana na awatendee fadhili kama mlivyowatendea hao waliofariki, na pia mimi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha Naomi akawaambia wakweze wawili, Nendeni sasa mkarejee kila mmoja nyumbani kwa mamaye; BWANA na awatendee mema ninyi, kama ninyi mlivyowatendea mema hao waliofariki na mimi pia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Naye Naomi akawaambia hao wakwe zake wawili, “Rudini kila mmoja nyumbani kwa mama yake. Naomba Mwenyezi-Mungu awe mwema kwenu kama mlivyokuwa wema kwangu na kwa wale watu wangu waliofariki.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naomi akawaambia wakwewe wawili: Nendeni kurudi kila mtu nyumbani mwa mama yake! Bwana awafanyizie mema, kama mlivyowafanyizia mema wanangu waliokufa, hata mimi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha Naomi akawaambia wakweze wawili, Nendeni sasa mkarejee kila mmoja nyumbani kwa mamaye; BWANA na awatendee mema ninyi, kama ninyi mlivyowatendea mema hao waliofariki na mimi pia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Naomi akawaambia hao wakwe zake wawili: “Murudi kila mumoja kwa mama yake. Ninaomba Yawe awatendee mema kama vile mulivyonitendea mema mimi na wale watu wangu waliokufa.