Ruth 2:11 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini Boazi akamjibu, “Nimeyasikia yote uliyomfanyia mama mkwe wako tangu mumeo afariki. Ninajua jinsi ulivyowaacha wazazi wako, ukaiacha nchi yako, na jinsi ulivyokuja kuishi kati ya watu ambao hukuwajua hapo awali.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Boazi akamjibu, “Nimeambiwa yote uliyomtendea mama mkwe wako tangu mume wako alipofariki, na jinsi ulivyomwacha baba yako na mama yako na nchi yako ulimozaliwa, ukaja kuishi na watu ambao hukuwafahamu awali.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye Boazi akajibu, akamwambia, Nimeelezwa sana yote uliyomfanyia mkweo, tangu alipokufa mumeo; na jinsi ulivyowaacha baba yako na mama yako, na nchi yako uliyozaliwa, ukawafikilia watu usiowajua tangu hapo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini Boazi akamjibu, “Nimeyasikia yote uliyomfanyia mama mkwe wako tangu mumeo afariki. Ninajua jinsi ulivyowaacha wazazi wako, ukaiacha nchi yako, na jinsi ulivyokuja kuishi kati ya watu ambao hukuwajua hapo awali.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Boazi akamjibu, “Nimeambiwa yote uliyomtendea mama mkwe wako tangu mume wake alipofariki, na jinsi ulivyomwacha baba yako na mama yako na nchi yako ulimozaliwa, ukaja kuishi na watu ambao hukuwafahamu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Boazi akamjibu, “Nimeambiwa yote uliyomtendea mama mkwe wako tangu mume wako alipofariki, na jinsi ulivyomwacha baba yako na mama yako na nchi yako ulimozaliwa, ukaja kuishi na watu ambao hukuwafahamu awali.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye Boazi akajibu, akamwambia, Nimeelezwa sana yote uliyomfanyia mkweo, tangu alipokufa mumeo; na jinsi ulivyowaacha baba yako na mama yako, na nchi yako uliyozaliwa, ukawafikia watu usiowajua tangu hapo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini Boazi akamjibu, “Nimeyasikia yote uliyomfanyia mama mkwe wako tangu mumeo afariki. Ninajua jinsi ulivyowaacha wazazi wako, ukaiacha nchi yako, na jinsi ulivyokuja kuishi kati ya watu ambao hukuwajua hapo awali.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Boazi akamjibu, akamwambia: Nimesimuliwa yote pia, uliyomfanyizia mkweo, mumeo alipokwisha kufa, ya kuwa umemwacha baba yako na mama yako na nchi, uliyozaliwa, ukaja kwa ukoo wa watu, usiowajua zamani zote.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye Boazi akajibu, akamwambia, Nimeelezwa sana yote uliyomfanyia mkweo, tangu alipokufa mumeo; na jinsi ulivyowaacha baba yako na mama yako, na nchi yako uliyozaliwa, ukawafikilia watu usiowajua tangu hapo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini Boazi akamujibu: “Nimeyasikia yote uliyomufanyia mama mukwe wako tangu mume wako alipokufa. Ninajua jinsi ulivyowaacha wazazi wako, ukaiacha inchi yako, na jinsi ulivyokuja kuishi kati ya watu ambao haukuwajua tangu zamani.