Ruth 2:12 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu akujaze kwa yote uliyoyafanya. Mwenyezi-Mungu wa Israeli uliyemkimbilia akulinde chini ya mabawa yake, akupe thawabu kamilifu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwenyezi Mungu na akulipe kwa yale uliyoyatenda. Ubarikiwe kwa wingi na Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, ambaye umekimbilia mabawani mwake.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana akujazi kwa kazi yako, nawe upewe thawabu kamili na Bwana, Mungu wa Israeli, ambaye umekuja kukimbilia chini ya mabawa yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu akujaze kwa yote uliyoyafanya. Mwenyezi-Mungu wa Israeli uliyemkimbilia akulinde chini ya mabawa yake, akupe thawabu kamilifu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
BWANA na akulipe kwa yale uliyoyatenda. Ubarikiwe kwa wingi na BWANA, Mungu wa Israeli, ambaye umekimbilia mbawani mwake.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
bwana na akulipe kwa yale uliyoyatenda. Ubarikiwe kwa wingi na bwana, Mungu wa Israeli, ambaye umekimbilia mabawani mwake.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
BWANA akujaze kwa kazi yako, nawe upewe thawabu kamili na BWANA, Mungu wa Israeli, ambaye umekuja kukimbilia chini ya mbawa zake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu akujaze kwa yote uliyoyafanya. Mwenyezi-Mungu wa Israeli uliyemkimbilia akulinde chini ya mabawa yake, akupe thawabu kamilifu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Bwana na akurudishie hayo matendo yako, upate mshahara wako wote mzima kwake Bwana Mungu wa Isiraeli, kwa kuwa umekuja kumkimbilia mabawani pake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
BWANA akujazi kwa kazi yako, nawe upewe thawabu kamili na BWANA, Mungu wa Israeli, ambaye umekuja kukimbilia chini ya mabawa yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe akubariki kwa yote uliyoyafanya. Yawe wa Israeli uliyemukimbilia akulinde chini ya mabawa yake, akupe zawadi kamilifu.”