Ruth 2:14 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakati wa chakula, Boazi alimkaribisha Ruthu akamwambia, “Karibu hapa, njoo ule mkate pia na uuchovye ndani ya divai.” Kwa hiyo Ruthu akaketi pamoja na wavunaji, na Boazi akampa nafaka iliyokaangwa, akala akashiba hata akabakiza.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakati wa chakula, Boazi akamwambia Ruthu, “Karibia hapa. Kula mkate na uchovye ndani ya siki.” Alipoketi pamoja na wavunaji, akampa nafaka zilizookwa. Akala kiasi alichotaka na kusaza.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena wakati wa chakula huyo Boazi akamwambia, Karibu kwetu, ule katika mkate wetu, na ulichovye tonge lako katika siki yetu. Basi akaketi pamoja na wavunaji, nao wakampitishia bisi, naye akala akashiba, hata akasaza.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakati wa chakula, Boazi alimkaribisha Ruthu akamwambia, “Karibu hapa, njoo ule mkate pia na uuchovye ndani ya divai.” Kwa hiyo Ruthu akaketi pamoja na wavunaji, na Boazi akampa nafaka iliyokaangwa, akala akashiba hata akabakiza.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati wa chakula Boazi akamwambia Ruthu, “Karibia hapa. Kula mkate na uchovye ndani ya divai.” Alipoketi pamoja na wavunaji, akampa nafaka zilizookwa. Akala kiasi alichotaka na kusaza.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati wa chakula, Boazi akamwambia Ruthu, “Karibia hapa. Kula mkate na uchovye ndani ya siki.” Alipoketi pamoja na wavunaji, akampa nafaka zilizookwa. Akala kiasi alichotaka na kusaza.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena wakati wa chakula huyo Boazi akamwambia, Karibu kwetu, ule katika mkate wetu, na ulichovye tonge lako katika siki yetu. Basi akaketi pamoja na wavunaji, nao wakampitishia bisi, naye akala akashiba, hata akasaza.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakati wa chakula, Boazi alimkaribisha Ruthu akamwambia, “Karibu hapa, njoo ule mkate pia na uuchovye ndani ya divai.” Kwa hiyo Ruthu akaketi pamoja na wavunaji, na Boazi akampa nafaka iliyokaangwa, akala akashiba hata akabakiza.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Saa wanapolia chakula, Boazi akamwambia: Karibu hapa, ule huku chakulani, nacho kitonge chako ukichovye hapa sikini! Akakaa kando ya wavunaji, naye akamgawia bisi, akala, hata akishiba, nyingine akazisaza.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena wakati wa chakula huyo Boazi akamwambia, Karibu kwetu, ule katika mkate wetu, na ulichovye tonge lako katika siki yetu. Basi akaketi pamoja na wavunaji, nao wakampitishia bisi, naye akala akashiba, hata akasaza.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakati wa chakula, Boazi akamukaribisha Ruta akamwambia: “Karibu hapa, kuja ukule mukate vilevile na uuchovye ndani ya divai.” Kwa hiyo Ruta akaikaa pamoja na wavunaji, na Boazi akamupa ngano iliyokaangwa, akakula akashiba hata akaacha sehemu.