Ruth 2:15 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Na ikawa Ruthu alipoendelea kuokota mavuno, Boazi aliwaambia wafanyakazi wake, “Mwacheni akusanye hata mahali miganda ilipo wala msimkemee.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Alipoinuka ili kuokota mabaki ya nafaka, Boazi akawaagiza watu wake, “Hata kama atakusanya kati ya miganda, msimzuie.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye alipoinuka tena ili aende kuokota masazo, huyo Boazi aliwaagiza vijana wake akisema, Mwacheni aokote hata kati ya miganda, wala msimkemee.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Na ikawa Ruthu alipoendelea kuokota mavuno, Boazi aliwaambia wafanyakazi wake, “Mwacheni akusanye hata mahali miganda ilipo wala msimkemee.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Alipoinuka ili kuokota mabaki ya nafaka, Boazi akawaagiza watu wake, “Hata kama atakusanya kati ya miganda, msimzuie.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Alipoinuka ili kuokota mabaki ya nafaka, Boazi akawaagiza watu wake, “Hata kama atakusanya kati ya miganda, msimzuie.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye alipoinuka tena ili aende kuokota masazo, huyo Boazi aliwaagiza vijana wake akisema, Mwacheni aokote hata kati ya miganda, wala msimkemee.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Na ikawa Ruthu alipoendelea kuokota mavuno, Boazi aliwaambia wafanyakazi wake, “Mwacheni akusanye hata mahali miganda ilipo wala msimkemee.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Alipoondoka kwenda kuokoteza, Boazi akawaagiza vijana wake kwamba: Hata katikati ya miganda na aokoteze, msimkaripie.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye alipoinuka tena ili aende kuokota masazo, huyo Boazi aliwaagiza vijana wake akisema, Mwacheni aokote hata kati ya miganda, wala msimkemee.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Naye Ruta alipoendelea kuokota mavuno, Boazi akawaambia watumishi wake: “Muache akusanye hata pahali miganda inapokuwa wala musimukaripie.