Ruth 2:19 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi mkwewe akamwuliza, “Uliokota wapi haya yote? Je, ulikuwa katika shamba la nani? Heri huyo aliyekufadhili.” Hapo Ruthu akamwambia Naomi kwamba alikuwa amefanya kazi katika shamba la mtu aliyeitwa Boazi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi mkwewe akamuuliza, “Je, umeokota wapi leo? Umefanya kazi wapi? Abarikiwe mtu yule aliyekujali.” Ndipo Ruthu akamwambia mama mkwe wake kuhusu mtu ambaye alikuwa amemfanyia kazi katika shamba lake. Akasema, “Yule mtu niliyefanyia kazi kwake leo, anaitwa Boazi.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi mkwewe akamwuliza, Je! Umeokota wapi leo? Umefanya kazi wapi? Na abarikiwe yeye aliyekufahamu. Naye akamwarifu mkwewe ni nani ambaye alifanya kazi kwake, akasema, Yule mtu niliyefanya kazi kwake leo jina lake aitwa Boazi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi mkwewe akamwuliza, “Uliokota wapi haya yote? Je, ulikuwa katika shamba la nani? Heri huyo aliyekufadhili.” Hapo Ruthu akamwambia Naomi kwamba alikuwa amefanya kazi katika shamba la mtu aliyeitwa Boazi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi mkwewe akamwuliza, “Je, umeokota wapi leo? Umefanya kazi wapi? Abarikiwe mtu yule aliyekujali.” Ndipo Ruthu akamwambia mama mkwe wake juu ya yule ambaye yeye alikuwa amefanyia kazi katika shamba lake. Akasema, “Yule mtu niliyefanyia kazi kwake leo, anaitwa Boazi.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi mkwewe akamuuliza, “Je, umeokota wapi leo? Umefanya kazi wapi? Abarikiwe mtu yule aliyekujali.” Ndipo Ruthu akamwambia mama mkwe wake juu ya yule ambaye yeye alikuwa amefanyia kazi katika shamba lake. Akasema, “Yule mtu niliyefanyia kazi kwake leo, anaitwa Boazi.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi mkwewe akamwuliza, Je! Umeokota wapi leo? Umefanya kazi wapi? Na abarikiwe yeye aliyekufahamu. Naye akamwarifu mkwewe ni nani ambaye alifanya kazi kwake, akasema, Yule mtu niliyefanya kazi kwake leo jina lake anaitwa Boazi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi mkwewe akamwuliza, “Uliokota wapi haya yote? Je, ulikuwa katika shamba la nani? Heri huyo aliyekufadhili.” Hapo Ruthu akamwambia Naomi kwamba alikuwa amefanya kazi katika shamba la mtu aliyeitwa Boazi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mkwewe akamwuliza: Umeokoteza wapi leo? Umekwenda wapi kufanya kazi? Aliyekuonea mema na abarikiwe! Akamsimulia mkwewe, kama ni nani, ambaye amezifanya kazi zake kwake, akasema: Jina la huyo mtu, ambaye nimezifanya leo kazi zangu kwake, ndiye Boazi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi mkwewe akamwuliza, Je! Umeokota wapi leo? Umefanya kazi wapi? Na abarikiwe yeye aliyekufahamu. Naye akamwarifu mkwewe ni nani ambaye alifanya kazi kwake, akasema, Yule mtu niliyefanya kazi kwake leo jina lake aitwa Boazi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi mama mukwe wake akamwuliza: “Uliokota wapi haya yote? Ulikuwa katika shamba la nani? Abarikiwe yule aliyekutendea wema.” Hapo Ruta akamwambia Naomi kwamba alikuwa akifanya kazi katika shamba la mutu aliyeitwa Boazi.