Ruth 2:20 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, Naomi akamwambia mkwewe, “Mwenyezi-Mungu ambariki Boazi! Mungu hutimiza daima ahadi zake kwa walio hai na waliokufa.” Kisha akaendelea kusema, “Huyo mtu ni ndugu yetu wa karibu na ni mmoja wa wale wenye wajibu wa kututunza.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Naye Naomi akamwambia mkwewe, “Mwenyezi Mungu ambariki! Hakuacha kuonesha fadhili zake kwa walio hai na kwa waliokufa.” Pia akamwambia, “Huyo mtu ni mmoja wa jamaa yetu wa karibu anayestahili kutukomboa.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye Naomi akamwambia mkwewe, Na abarikiwe huyo na Bwana, ambaye hakuuacha wema wake, wala kwa hao walio hai wala kwao waliokufa. Kisha Naomi akamwambia, Mtu huyu ni wa mbari yetu, mmojawapo wa jamaa yetu aliye karibu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, Naomi akamwambia mkwewe, “Mwenyezi-Mungu ambariki Boazi! Mungu hutimiza daima ahadi zake kwa walio hai na waliokufa.” Kisha akaendelea kusema, “Huyo mtu ni ndugu yetu wa karibu na ni mmoja wa wale wenye wajibu wa kututunza.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Naye Naomi akamwambia mkwewe, “BWANA ambariki! Hakuacha kuonyesha fadhili zake kwa walio hai na kwa hao waliokufa.” Pia akamwambia, “Huyo mtu ni mmoja wa jamaa yetu wa karibu anayestahili kukomboa.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Naye Naomi akamwambia mkwewe, “ bwana ambariki! Hakuacha kuonyesha fadhili zake kwa walio hai na kwa waliokufa.” Pia akamwambia, “Huyo mtu ni mmoja wa jamaa yetu wa karibu anayestahili kutukomboa.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye Naomi akamwambia mkwewe, Na abarikiwe huyo na BWANA, ambaye hakuuacha wema wake, wala kwa hao walio hai wala kwa waliokufa. Kisha Naomi akamwambia, Mtu huyu ni wa ukoo wetu, mmojawapo wa jamaa yetu aliye karibu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, Naomi akamwambia mkwewe, “Mwenyezi-Mungu ambariki Boazi! Mungu hutimiza daima ahadi zake kwa walio hai na waliokufa.” Kisha akaendelea kusema, “Huyo mtu ni ndugu yetu wa karibu na ni mmoja wa wale wenye wajibu wa kututunza.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, Naomi alipomjibu mkwewe: Na abarikiwe na Bwana! Kwa kuwa hakuacha kuwatolea mema, wala wazima, wala wafu. Naomi akamwambia tena: Mtu huyo ni ndugu yetu, naye ni mmoja wa waingiliaji wetu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye Naomi akamwambia mkwewe, Na abarikiwe huyo na BWANA, ambaye hakuuacha wema wake, wala kwa hao walio hai wala kwao waliokufa. Kisha Naomi akamwambia, Mtu huyu ni wa mbari yetu, mmojawapo wa jamaa yetu aliye karibu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, Naomi akamwambia mukwe wake: “Yawe amubariki Boazi! Mungu anatimiza siku zote ahadi zake kwa wanaokuwa wazima na waliokufa.” Kisha akaendelea kusema: “Huyo mutu ni ndugu yetu wa karibu na ni mumoja wa wale wenye mapaswa ya kututunza.”