Ruth 2:22 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, Naomi akamwambia Ruthu, “Naam binti yangu. Ni vyema kufanya kazi pamoja na wanawake wengine katika shamba la Boazi, kwa maana labda ungesumbuliwa kama ungekwenda katika shamba la mtu mwingine.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha Naomi akamwambia Ruthu mkwewe, “Binti yangu, itakuwa vyema wewe ufuatane na wajakazi wake, kwa sababu katika shamba la mtu mwingine wanaweza kukudhuru.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha Naomi akamwambia Ruthu mkwewe, Mwanangu, ni vizuri wewe ufuatane na wasichana wake, wala watu wasikukute katika konde linginelo lote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, Naomi akamwambia Ruthu, “Naam binti yangu. Ni vyema kufanya kazi pamoja na wanawake wengine katika shamba la Boazi, kwa maana labda ungesumbuliwa kama ungekwenda katika shamba la mtu mwingine.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha Naomi akamwambia Ruthu mkwewe, “Binti yangu, itakuwa vyema wewe ufuatane na wasichana wake, kwa sababu katika shamba la mtu mwingine wanaweza kukudhuru.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha Naomi akamwambia Ruthu mkwewe, “Binti yangu, itakuwa vyema wewe ufuatane na wasichana wake, kwa sababu katika shamba la mtu mwingine wanaweza kukudhuru.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha Naomi akamwambia Ruthu mkwewe, Mwanangu, ni vizuri wewe ufuatane na wasichana wake, ili watu wasikusumbue katika shamba lingine lolote lile.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, Naomi akamwambia Ruthu, “Naam binti yangu. Ni vyema kufanya kazi pamoja na wanawake wengine katika shamba la Boazi, kwa maana labda ungesumbuliwa kama ungekwenda katika shamba la mtu mwingine.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naomi akamjibu mkwewe Ruti: Inafaa, mwanangu, ukitoka pamoja na vijakazi wake, wasikukaripie halafu shambani.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha Naomi akamwambia Ruthu mkwewe, Mwanangu, ni vizuri wewe ufuatane na wasichana wake, wala watu wasikukute katika konde linginelo lote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, Naomi akamwambia Ruta: “Hakika binti yangu, ni vizuri kufanya kazi pamoja na wanawake wengine katika shamba la Boazi, kwa maana labda ungesumbuliwa kama ungekwenda katika shamba la mutu mwingine.”