Ruth 2:3 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi Ruthu akaenda shambani, akawafuata wavunaji huku anayaokota masuke waliyoyaacha. Na kumbe akajikuta katika shamba la Boazi, yule wa ukoo wake Elimeleki.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi akaenda, akaokota mabaki ya nafaka mashambani nyuma ya wavunaji. Ikatokea kwamba alijikuta akifanya kazi kwenye shamba lililokuwa mali ya Boazi, ambaye alikuwa wa ukoo wa Elimeleki.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi akaenda, akaja akaokota masazo kondeni nyuma ya wavunaji; na bahati yake ikamtukia kwamba akaifika sehemu ya shamba iliyokuwa mali yake huyo Boazi, ambaye alikuwa wa jamaa yake Elimeleki.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi Ruthu akaenda shambani, akawafuata wavunaji huku anayaokota masuke waliyoyaacha. Na kumbe akajikuta katika shamba la Boazi, yule wa ukoo wake Elimeleki.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi akaenda, akaokota mabaki ya nafaka nyuma ya wavunaji. Ikatokea kwamba alijikuta anafanya kazi kwenye shamba lililokuwa mali ya Boazi, ambaye alitoka kwenye ukoo wa Elimeleki.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi akaenda, akaokota mabaki ya nafaka mashambani nyuma ya wavunaji. Ikatokea kwamba alijikuta anafanya kazi kwenye shamba lililokuwa mali ya Boazi, ambaye alitoka kwenye ukoo wa Elimeleki.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi akaenda, akaja akaokota mabaki shambani nyuma ya wavunaji; na kwa bahati akafikia sehemu ya shamba la Boazi, ambaye alikuwa wa jamaa yake Elimeleki.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi Ruthu akaenda shambani, akawafuata wavunaji huku anayaokota masuke waliyoyaacha. Na kumbe akajikuta katika shamba la Boazi, yule wa ukoo wake Elimeleki.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akaenda, akaja kuokoteza shambani akiwafuata wavunaji. Ikatukia kwa bahati, lile fugu la shamba kuwa lake Boazi aliyekuwa wa mlango wa Elimeleki.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi akaenda, akaja akaokota masazo kondeni nyuma ya wavunaji; na bahati yake ikamtukia kwamba akaifika sehemu ya shamba iliyokuwa mali yake huyo Boazi, ambaye alikuwa wa jamaa yake Elimeleki.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi Ruta akaenda katika shamba, akawafuata wavunaji naye akiyaokota masuke waliyoyaacha. Na kumbe akajikuta katika shamba la Boazi, yule wa ukoo wa Elimeleki.