Ruth 3:10 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Boazi akasema, “Mwenyezi-Mungu na akubariki, kwa maana kwa yote unayofanya unaonesha heshima zaidi kuliko uliyoyafanya hapo awali, kwa maana hukuwatafuta vijana maskini au tajiri wakuoe.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akamwambia, “Binti yangu, ubarikiwe na Mwenyezi Mungu. Wema huu wa sasa ni mkuu kushinda hata ule ulioonesha mwanzoni. Hukuwakimbilia vijana, wakiwa matajiri au maskini.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akamwambia, Mwanangu, ubarikiwe na Bwana; umezidi kuonyesha fadhili zako mwisho kuliko mwanzo, kwa vile usivyowafuata vijana, kama ni maskini kama ni matajiri.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Boazi akasema, “Mwenyezi-Mungu na akubariki, kwa maana kwa yote unayofanya unaonesha heshima zaidi kuliko uliyoyafanya hapo awali, kwa maana hukuwatafuta vijana maskini au tajiri wakuoe.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akamwambia, “Binti yangu, ubarikiwe na BWANA. Wema huu wa sasa ni mkuu kushinda hata ule ulioonyesha mwanzoni. Hukuwakimbilia vijana, wakiwa matajiri au maskini.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akamwambia, “Binti yangu, ubarikiwe na bwana. Wema huu wa sasa ni mkuu kushinda hata ule ulioonyesha mwanzoni. Hukuwakimbilia vijana, wakiwa matajiri au maskini.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akamwambia, Mwanangu, ubarikiwe na BWANA; umezidi kuonesha fadhili zako mwisho kuliko mwanzo, kwa vile usivyowafuata vijana, wawe ni maskini au matajiri.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Boazi akasema, “Mwenyezi-Mungu na akubariki, kwa maana kwa yote unayofanya unaonesha heshima zaidi kuliko uliyoyafanya hapo awali, kwa maana hukuwatafuta vijana maskini au tajiri wakuoe.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akamjibu: Na ubarikiwe na Bwana, mwanangu! Haya mema yako ya nyuma, uliyoyafanya, yanayapita ya kwanza kwa wema, usipowafuata vijana, kama ni maskini au kama ni wenye mali.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akamwambia, Mwanangu, ubarikiwe na BWANA; umezidi kuonyesha fadhili zako mwisho kuliko mwanzo, kwa vile usivyowafuata vijana, kama ni maskini kama ni matajiri.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Boazi akasema: “Yawe akubariki, kwa maana kwa yote unayofanya unaonyesha heshima zaidi kuliko uliyoyafanya pale mbele, kwa maana haukuwatafuta vijana wamasikini au tajiri wakuoe.