Ruth 3:11 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sasa binti yangu usifadhaike, nitakufanyia lolote utakaloomba kwa kuwa kila mtu mjini humu anajua wema wako.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Sasa, binti yangu, usiogope. Nitakufanyia yote uliyoomba. Kwa maana mji wote wa watu wangu wanakujua kwamba wewe ni mwanamke mwenye tabia nzuri.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi, mwanangu, usiogope; mimi nitakufanyia yote uyanenayo; kwa maana mji wote pia wa watu wangu wanakujua ya kwamba u mwanamke mwema.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sasa binti yangu usifadhaike, nitakufanyia lolote utakaloomba kwa kuwa kila mtu mjini humu anajua wema wako.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Sasa, binti yangu, usiogope. Nitakufanyia yote uliyoomba. Kwa maana mji wote wa watu wangu wanakujua ya kwamba wewe ni mwanamke mwenye tabia nzuri.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Sasa, binti yangu, usiogope. Nitakufanyia yote uliyoomba. Kwa maana mji wote wa watu wangu wanakujua ya kwamba wewe ni mwanamke mwenye tabia nzuri.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi, mwanangu, usiogope; mimi nitakufanyia yote uyanenayo; kwa maana watu wote wa mjini wangu wanakujua ya kwamba u mwanamke mwema.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Sasa binti yangu usifadhaike, nitakufanyia lolote utakaloomba kwa kuwa kila mtu mjini humu anajua wema wako.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Sasa mwanangu, usiogope! Yote, utakayoniambia, nitakufanyizia; kwani watu wangu wote waliomo malangoni mwangu wanakujua wewe kuwa mwanamke mwema sana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi, mwanangu, usiogope; mimi nitakufanyia yote uyanenayo; kwa maana mji wote pia wa watu wangu wanakujua ya kwamba u mwanamke mwema.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Sasa binti yangu usifazaike, nitakufanyia lolote utakaloomba kwa sababu kila mutu katika muji huu anajua wema wako.