Ruth 3:13 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa hiyo, kaa hapa usiku wote, na kesho asubuhi tutaona kama atakubali kukutunza au la. Ikiwa atakutunza ni vyema. Akikataa, kwa jina la Mwenyezi-Mungu aliye hai mimi nitakutunza. Lala hapa mpaka asubuhi.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wewe kaa hapa usiku huu, kisha asubuhi akikubali kukukomboa, vyema, na akomboe. La sivyo, kama hayuko tayari, hakika kama Mwenyezi Mungu aishivyo nitafanya hivyo. Lala hapa hadi asubuhi.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wewe ungoje usiku huu; kisha, asubuhi, kama akikubali kukufanyia impasavyo jamaa, haya, na akufanyie; lakini ikiwa hataki yeye, basi mimi nitakufanyia impasavyo jamaa; Bwana aishivyo. Ulale wewe hata asubuhi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa hiyo, kaa hapa usiku wote, na kesho asubuhi tutaona kama atakubali kukutunza au la. Ikiwa atakutunza ni vyema. Akikataa, kwa jina la Mwenyezi-Mungu aliye hai mimi nitakutunza. Lala hapa mpaka asubuhi.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wewe kaa hapa usiku huu, kisha asubuhi kama akikubali kukomboa, vyema na akomboe. La sivyo kama hayuko tayari, hakika kama BWANA aishivyo nitafanya hivyo. Lala hapa mpaka asubuhi.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wewe kaa hapa usiku huu, kisha asubuhi kama akikubali kukomboa, vyema na akomboe. La sivyo kama hayuko tayari, hakika kama bwana aishivyo nitafanya hivyo. Lala hapa mpaka asubuhi.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wewe ungoje usiku huu; kisha, asubuhi, kama akikubali kukufanyia impasavyo jamaa, haya, na akufanyie; lakini ikiwa hataki yeye, basi mimi nitakufanyia impasavyo jamaa; BWANA aishivyo. Ulale wewe hadi asubuhi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa hiyo, kaa hapa usiku wote, na kesho asubuhi tutaona kama atakubali kukutunza au la. Ikiwa atakutunza ni vyema. Akikataa, kwa jina la Mwenyezi-Mungu aliye hai mimi nitakutunza. Lala hapa mpaka asubuhi.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Usiku huu lala hapa! Kesho asubuhi itajulikana: akiwa anataka kukuingilia, basi, ni vema, na akuingilie! Lakini akiwa hataki kukuingilia, mimi nitakuingilia kwa hivyo, Bwana alivyo Mwenye uzima! Lala tu, mpaka kuche!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wewe ungoje usiku huu; kisha, asubuhi, kama akikubali kukufanyia impasavyo jamaa, haya, na akufanyie; lakini ikiwa hataki yeye, basi mimi nitakufanyia impasavyo jamaa; BWANA aishivyo. Ulale wewe hata asubuhi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa hiyo, kaa hapa usiku wote, na kesho asubui tutaona kama atakubali kukutunza au hapana. Ikiwa atakutunza ni vizuri. Kama vile Yawe anavyoishi, akikataa, mimi nitakutunza. Lala hapa mpaka asubui.”