Ruth 3:14 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi Ruthu akalala hapo miguuni pake mpaka asubuhi, lakini aliamka alfajiri ili asionekane, kwa kuwa Boazi hakutaka mtu ajue kuwa Ruthu alikuwa mahali pa kupuria.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivyo huyo mwanamke akalala miguuni pake hadi asubuhi, akaondoka mapema pasipo mtu kuweza kumtambua mwenzake, maana Boazi alisema, “Isijulikane kabisa ya kuwa mwanamke alifika kwenye sakafu ya kupuria.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hivyo huyo mwanamke akalala miguuni pake hata asubuhi; akaondoka mapema asijaweza mtu kumtambua mwenziwe; maana Boazi amesema, Isijulikane kabisa ya kuwa mwanamke alifika penye uga.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi Ruthu akalala hapo miguuni pake mpaka asubuhi, lakini aliamka alfajiri ili asionekane, kwa kuwa Boazi hakutaka mtu ajue kuwa Ruthu alikuwa mahali pa kupuria.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivyo huyo mwanamke akalala miguuni pake mpaka asubuhi, akaondoka mapema asijaweza mtu kumtambua mwenzake, maana Boazi alisema, “Isijulikane kabisa ya kuwa mwanamke alifika kwenye sakafu ya kupuria.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivyo huyo mwanamke akalala miguuni pake mpaka asubuhi, akaondoka mapema pasipo mtu kuweza kumtambua mwenzake, maana Boazi alisema, “Isijulikane kabisa ya kuwa mwanamke alifika kwenye sakafu ya kupuria.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hivyo huyo mwanamke akalala miguuni pake hata asubuhi; akaondoka mapema asijaweza mtu kumtambua mwenziwe; maana Boazi amesema, Isijulikane kabisa ya kuwa mwanamke alifika penye uga.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi Ruthu akalala hapo miguuni pake mpaka asubuhi, lakini aliamka alfajiri ili asionekane, kwa kuwa Boazi hakutaka mtu ajue kuwa Ruthu alikuwa mahali pa kupuria.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akalala miguuni pake, hata kulipokucha; akaamka hapo, mtu asipoweza bado kumtambua mwenzake; Boazi akamwambia: Isijulikane, ya kuwa mwanamke amefika hapa pa kupuria!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hivyo huyo mwanamke akalala miguuni pake hata asubuhi; akaondoka mapema asijaweza mtu kumtambua mwenziwe; maana Boazi amesema, Isijulikane kabisa ya kuwa mwanamke alifika penye uga.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi Ruta akalala pale kwenye miguu yake mpaka asubui, lakini akaamuka asubui mapema kusudi asionekane, kwa sababu Boazi hakutaka mutu ajue kwamba Ruta alikuwa kwenye kiwanja cha kupepetea.