Ruth 3:7 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Boazi alipomaliza kula na kunywa, akafurahi moyoni. Basi alikwenda karibu na tita la shayiri, akalala. Ruthu alikwenda polepole akafunua miguu yake na kulala hapo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Boazi alipomaliza kula na kunywa, naye akawa amejawa na furaha, alienda kulala mwisho wa lundo la nafaka. Ruthu akanyemelea polepole, akafunua miguu yake, na akalala.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ikawa huyo Boazi alipokwisha kula na kunywa, na moyo wake umekunjuka, alikwenda kulala penye mwisho wa chungu ya nafaka; na huyo mwanamke akaja taratibu, akaifunua miguu yake, akajilaza papo hapo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Boazi alipomaliza kula na kunywa, akafurahi moyoni. Basi alikwenda karibu na tita la shayiri, akalala. Ruthu alikwenda polepole akafunua miguu yake na kulala hapo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati Boazi alipomaliza kula na kunywa, naye alikuwa amejawa na furaha, alikwenda kulala mwisho wa lundo la nafaka. Ruthu akakaribia kimya kimya, akafunua miguu yake, akalala.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati Boazi alipomaliza kula na kunywa, naye akawa amejawa na furaha, alikwenda kulala mwisho wa lundo la nafaka. Ruthu akanyemelea polepole, akafunua miguu yake, na akalala.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ikawa huyo Boazi alipokwisha kula na kunywa, na moyo wake umekunjuka, alikwenda kulala penye mwisho wa rundo la nafaka; na huyo mwanamke akaja taratibu, akaifunua miguu yake, akajilaza papo hapo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Boazi alipomaliza kula na kunywa, akafurahi moyoni. Basi alikwenda karibu na tita la shayiri, akalala. Ruthu alikwenda polepole akafunua miguu yake na kulala hapo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Boazi akala, akanywa, moyo wake ukachangamka, kisha akaenda kulala nyuma ya chungu la miganda. Ndipo, alipokwenda hapo polepole, akaifunua miguu yake, akalala naye.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ikawa huyo Boazi alipokwisha kula na kunywa, na moyo wake umekunjuka, alikwenda kulala penye mwisho wa chungu ya nafaka; na huyo mwanamke akaja taratibu, akaifunua miguu yake, akajilaza papo hapo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Boazi alipomaliza kula na kunywa, akachangamuka. Akakwenda karibu na lundo la shayiri, akalala. Ruta akakwenda polepole akafunua miguu yake na kulala pale.