Ruth 4:1 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Boazi alikwenda mahali pa kufanyia mkutano huko kwenye lango la mji akaketi chini. Kisha yule ndugu ya Elimeleki ambaye Boazi alikuwa amemtaja, akapita karibu na hapo. Boazi akamwita, akasema, “Njoo, uketi hapa ndugu.” Basi huyo mtu akaja na kuketi hapo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Boazi akakwea hadi lango la mji, akaketi pale. Yule mtu wa jamaa aliyekuwa wa karibu wa kukomboa, ambaye Boazi alimtaja, akaja. Boazi akasema, “Njoo hapa, rafiki yangu. Karibu uketi.” Naye akakaribia, akaketi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi Boazi akakwea kwenda mpaka langoni, akaketi pale; na tazama, yule mtu wa jamaa aliyekuwa karibu, ambaye Boazi amemnena, akapita. Naye akamwita, Haya! Wewe, karibu, uketi hapa. Naye akaja akaketi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Boazi alikwenda mahali pa kufanyia mkutano huko kwenye lango la mji akaketi chini. Kisha yule ndugu ya Elimeleki ambaye Boazi alikuwa amemtaja, akapita karibu na hapo. Boazi akamwita, akasema, “Njoo, uketi hapa ndugu.” Basi huyo mtu akaja na kuketi hapo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Boazi akakwea mpaka kwenye lango la mji, akaketi pale. Kisha muda si mrefu yule mtu wa jamaa aliyekuwa wa karibu wa kukomboa, ambaye Boazi alimtaja, akaja. Boazi akasema, “Njoo hapa rafiki yangu, karibu uketi.” Naye akakaribia, akaketi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Boazi akakwea mpaka kwenye lango la mji, akaketi pale. Yule mtu wa jamaa aliyekuwa wa karibu wa kukomboa, ambaye Boazi alimtaja, akaja. Boazi akasema, “Njoo hapa, rafiki yangu. Karibu uketi.” Naye akakaribia, akaketi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi Boazi akakwea kwenda mpaka langoni, akaketi pale; na tazama, yule mtu wa jamaa aliyekuwa karibu, ambaye Boazi amemnena, akapita. Naye akamwita, Haya! Wewe, karibu, uketi hapa. Naye akaja akaketi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Boazi alikwenda mahali pa kufanyia mkutano huko kwenye lango la mji akaketi chini. Kisha yule ndugu ya Elimeleki ambaye Boazi alikuwa amemtaja, akapita karibu na hapo. Boazi akamwita, akasema, “Njoo, uketi hapa ndugu.” Basi huyo mtu akaja na kuketi hapo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Boazi akapanda kwenda langoni pa mji, akakaa huko. Mara yule mwingiliaji, Boazi aliyemtaja, akapita; ndipo, alipomwambia: Njoo, wewe bwana fulani, ukae hapa! Akaacha kwenda, akaja kukaa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi Boazi akakwea kwenda mpaka langoni, akaketi pale; na tazama, yule mtu wa jamaa aliyekuwa karibu, ambaye Boazi amemnena, akapita. Naye akamwita, Haya! Wewe, karibu, uketi hapa. Naye akaja akaketi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Boazi akakwenda kwa nafasi ya kufanyia mukutano kule kwenye mulango wa muji, akaikaa chini. Kisha yule ndugu ya Elimeleki ambaye Boazi alikuwa amemutaja, akapita karibu na pale. Boazi akamwita, akasema: “Kuja, uikae hapa ndugu.” Basi yule mutu akakuja na kuikaa pale.