Ruth 4:11 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi wazee waliokuwa langoni na watu wote waliokuwapo walijibu, “Ndiyo, sisi ni mashahidi. Mwenyezi-Mungu amfanye mke wako awe kama Raheli na Lea, ambao wote wawili waliijenga nyumba ya Israeli. Nawe upate kustawi katika jamaa ya Efratha, uwe na sifa katika Bethlehemu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha wazee pamoja na watu wote waliokuwa langoni wakasema, “Sisi ni mashahidi. Mwenyezi Mungu na amfanye mwanamke huyu aingiaye nyumbani mwako kuwa kama Raheli na kama Lea, wale wanawake wawili ambao pamoja waliijenga nyumba ya Israeli. Nawe ufanikiwe katika Efrata na uwe mashuhuri katika Bethlehemu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na watu wote waliokuwapo langoni, na wale wazee, wakasema, Naam, sisi ni mashahidi. Bwana na amfanye mwanamke huyu aingiaye nyumbani mwako kuwa kama Raheli na kama Lea, wale wawili walioijenga nyumba ya Israeli. Nawe ufanikiwe katika Efrata, na kuwa mashuhuri katika Bethlehemu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi wazee waliokuwa langoni na watu wote waliokuwapo walijibu, “Ndiyo, sisi ni mashahidi. Mwenyezi-Mungu amfanye mke wako awe kama Raheli na Lea, ambao wote wawili waliijenga nyumba ya Israeli. Nawe upate kustawi katika jamaa ya Efratha, uwe na sifa katika Bethlehemu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha wazee pamoja na watu wote waliokuwa langoni wakasema, “Sisi ni mashahidi. BWANA na amfanye mwanamke huyu aingiaye nyumbani mwako kuwa kama Raheli na kama Lea, wale wanawake wawili ambao kwa pamoja waliijenga nyumba ya Israeli. Nawe ufanikiwe katika Efrathi na uwe mashuhuri katika Bethlehemu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha wazee pamoja na watu wote waliokuwa langoni wakasema, “Sisi ni mashahidi. bwana na amfanye mwanamke huyu aingiaye nyumbani mwako kuwa kama Raheli na kama Lea, wale wanawake wawili ambao pamoja waliijenga nyumba ya Israeli. Nawe ufanikiwe katika Efrathi na uwe mashuhuri katika Bethlehemu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na watu wote waliokuwapo langoni, na wale wazee, wakasema, Naam, sisi ni mashahidi. BWANA na amfanye mwanamke huyu aingiaye nyumbani mwako kuwa kama Raheli na kama Lea, wale wawili walioijenga nyumba ya Israeli. Nawe ufanikiwe katika Efrata, na kuwa mashuhuri katika Bethlehemu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi wazee waliokuwa langoni na watu wote waliokuwapo walijibu, “Ndiyo, sisi ni mashahidi. Mwenyezi-Mungu amfanye mke wako awe kama Raheli na Lea, ambao wote wawili waliijenga nyumba ya Israeli. Nawe upate kustawi katika jamaa ya Efratha, uwe na sifa katika Bethlehemu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, watu wote waliokuwako malangoni nao wazee wale waliposema: Tu mashahidi. Bwana na amfanye huyu mwanamke aliyeingia nyumbani mwako kuwa kama Raheli na kama Lea walioijenga wote wawili nyumba ya Isiraeli! Pata nguvu mle Efurata, jina lako litajwe mle Beti-Lehemu!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na watu wote waliokuwapo langoni, na wale wazee, wakasema, Naam, sisi ni mashahidi. BWANA na amfanye mwanamke huyu aingiaye nyumbani mwako kuwa kama Raheli na kama Lea, wale wawili walioijenga nyumba ya Israeli. Nawe ufanikiwe katika Efrata, na kuwa mashuhuri katika Bethlehemu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi wazee waliokuwa kwenye mulango na watu wote waliokuwa pale wakajibu: “Ndiyo, sisi ni washuhuda. Yawe amufanye muke wako akuwe kama Rakeli na Lea, ambao wote wawili waliijenga nyumba ya Israeli. Nawe upate kustawi katika jamaa ya Efurata, ukuwe na sifa katika Betelehemu.