Ruth 4:12 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa sababu ya watoto Mwenyezi-Mungu atakaokupatia ambao mwanamke huyu atakuzalia, nayo nyumba yako iwe kama nyumba ya Peresi ambaye Tamari alimzalia Yuda.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kupitia kwa uzao ambao Mwenyezi Mungu atakupa kutokana na huyu mwanamwali, jamaa yako na ifanane na ya Peresi, ambaye Tamari alimzalia Yuda.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nyumba yako na ifanane na nyumba yake Peresi, ambaye kwamba Tamari alimzalia Yuda, kwa wazao atakaokupa Bwana katika mwanamke huyu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa sababu ya watoto Mwenyezi-Mungu atakaokupatia ambao mwanamke huyu atakuzalia, nayo nyumba yako iwe kama nyumba ya Peresi ambaye Tamari alimzalia Yuda.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kupitia kwa watoto ambao BWANA atakupa kutokana na huyu mwanamke kijana, jamaa yako na ifanane na ya Peresi, ambaye Tamari alimzalia Yuda.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kupitia kwa watoto ambao bwana atakupa kutokana na huyu mwanamwali, jamaa yako na ifanane na ya Peresi, ambaye Tamari alimzalia Yuda.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nyumba yako na ifanane na nyumba yake Peresi, ambaye Tamari alimzalia Yuda, kwa wazao atakaokupa BWANA katika mwanamke huyu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa sababu ya watoto Mwenyezi-Mungu atakaokupatia ambao mwanamke huyu atakuzalia, nayo nyumba yako iwe kama nyumba ya Peresi ambaye Tamari alimzalia Yuda.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao mlango wako uwe kama mlango wa Peresi, Tamari aliyemzalia Yuda, nao utoke katika wazao, Bwana atakaokupa kwa kijana huyu!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nyumba yako na ifanane na nyumba yake Peresi, ambaye kwamba Tamari alimzalia Yuda, kwa wazao atakaokupa BWANA katika mwanamke huyu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe akupatie watoto wengi kwa njia ya mwanamuke huyu, na jamaa yako ikuwe kama ya Peresi ambaye Tamari alimuzalia Yuda.”