Ruth 4:6 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yule jamaa aliyekuwa wa karibu akajibu, “Ikiwa ni hivyo, sitalifidia shamba hilo, kwa sababu yaonekana kuwa nitauharibu urithi wangu. Afadhali haki yangu ya kulichukua nikupe wewe, maana mimi siwezi kulifidia.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Aliposikia hili, yule jamaa wa karibu wa kukomboa akasema, “Basi mimi sitaweza kuikomboa, kwa sababu inaonekana nitauhatarisha urithi wangu. Wewe ikomboe mwenyewe. Mimi sitaweza.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi yule jamaa aliyekuwa wa karibu akasema, Mimi sitaweza kulikomboa kwa nafsi yangu, nisije nikauharibu urithi wangu mwenyewe; basi haki yangu ya kulikomboa ujichukulie wewe, maana mimi sitaweza kulikomboa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yule jamaa aliyekuwa wa karibu akajibu, “Ikiwa ni hivyo, sitalifidia shamba hilo, kwa sababu yaonekana kuwa nitauharibu urithi wangu. Afadhali haki yangu ya kulichukua nikupe wewe, maana mimi siwezi kulifidia.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kuhusu hili, yule jamaa wa karibu wa kukomboa akasema, “Basi mimi sitaweza kukomboa kwa sababu inaonekana nitauhatarisha urithi wangu. Wewe komboa mwenyewe. Mimi sitaweza.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Aliposikia hili, yule jamaa wa karibu wa kukomboa akasema, “Basi mimi sitaweza kuikomboa, kwa sababu inaonekana nitauhatarisha urithi wangu. Wewe ikomboe mwenyewe. Mimi sitaweza.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi yule jamaa aliyekuwa wa karibu akasema, Mimi sitaweza kulikomboa kwa nafsi yangu, nisije nikauharibu urithi wangu mwenyewe; basi haki yangu ya kulikomboa ujichukulie wewe, maana mimi sitaweza kulikomboa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yule jamaa aliyekuwa wa karibu akajibu, “Ikiwa ni hivyo, sitalifidia shamba hilo, kwa sababu yaonekana kuwa nitauharibu urithi wangu. Afadhali haki yangu ya kulichukua nikupe wewe, maana mimi siwezi kulifidia.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, yule mwingiliaji aliposema: Sitaweza kulikomboa, liwe langu, nisiliharibu fungu langu. Likomboe wewe, liwe lako lililonipasa mimi, nilikomboe. Kwani siwezi kulikomboa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi yule jamaa aliyekuwa wa karibu akasema, Mimi sitaweza kulikomboa kwa nafsi yangu, nisije nikauharibu urithi wangu mwenyewe; basi haki yangu ya kulikomboa ujichukulie wewe, maana mimi sitaweza kulikomboa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yule ndugu aliyekuwa wa karibu akajibu: “Ikiwa ni hivyo, sitalikomboa shamba hilo, kwa sababu inaonekana kwamba nitauharibu urizi wangu. Afazali nikupe wewe haki yangu ya kulikomboa, maana mimi siwezi kulikomboa.”