Ruth 4:7 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Siku zile, katika Israeli ikiwa watu walitaka kukomboa au kubadilishana kitu, ilikuwa ni desturi kwa mtu kuonesha ishara kwa kuvua kiatu chake na kumpa mwingine. Kwa ishara hiyo Waisraeli walionesha kwamba mambo yamesawazishwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
(Basi katika siku za kale huko Israeli, ili kukamilisha tendo la kukomboa na kukabidhiana mali, mmoja huvua kiatu chake na kumpatia mwingine. Hii ilikuwa ni njia ya kuhalalisha mabadilishano katika Israeli.)
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi hii ilikuwa desturi zamani za kale katika Israeli, kwa habari ya kukomboa na kubadiliana, ili kuyahakikisha yote; mtu huvua kiatu chake na kumpa mwenziwe; ndivyo walivyohakikisha neno katika Israeli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Siku zile, katika Israeli ikiwa watu walitaka kukomboa au kubadilishana kitu, ilikuwa ni desturi kwa mtu kuonesha ishara kwa kuvua kiatu chake na kumpa mwingine. Kwa ishara hiyo Waisraeli walionesha kwamba mambo yamesawazishwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
(Basi katika siku za kale huko Israeli, ili kukamilisha tendo la kukomboa na kukabidhiana mali, mmoja huvua kiatu chake na kumpatia mwingine. Hii ilikuwa ni njia ya kuhalalisha mabadilishano katika Israeli.)
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
(Basi katika siku za kale huko Israeli, ili kukamilisha tendo la kukomboa na kukabidhiana mali, mmoja huvua kiatu chake na kumpatia mwingine. Hii ilikuwa ni njia ya kuhalalisha mabadilishano katika Israeli.)
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi hii ilikuwa desturi zamani za kale katika Israeli, kwa habari ya kukomboa na kubadilishana, ili kuyahakikisha yote; mtu huvua kiatu chake na kumpa mwenziwe; ndivyo walivyohakikisha neno katika Israeli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Siku zile, katika Israeli ikiwa watu walitaka kukomboa au kubadilishana kitu, ilikuwa ni desturi kwa mtu kuonesha ishara kwa kuvua kiatu chake na kumpa mwingine. Kwa ishara hiyo Waisraeli walionesha kwamba mambo yamesawazishwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tena kale kwa Waisiraeli ilikuwa desturi, walipokomboa, au waliponunua shamba, wakitaka kulishupaza hilo jambo la namna hii, mtu avue kiatu chake kimoja, ampe mwenzake; huu ulikuwa ushuhuda kwao Waisiraeli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi hii ilikuwa desturi zamani za kale katika Israeli, kwa habari ya kukomboa na kubadiliana, ili kuyahakikisha yote; mtu huvua kiatu chake na kumpa mwenziwe; ndivyo walivyohakikisha neno katika Israeli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Siku zile katika Israeli, kama watu walitaka kukomboa au kubadilishana kitu, ilikuwa desturi kwa mutu kuonyesha kitambulisho kwa kuvua kiatu chake na kumupa mwingine. Kwa kitambulisho hicho, Waisraeli walionyesha kwamba mambo yamesawazishwa.