Song of Solomon 1:4 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nichukue, twende zetu haraka, mfalme amenileta katika chumba chake. Tutafurahi na kushangilia kwa sababu yako, tutasifu mapenzi yako kuliko divai. Wanawake wana haki kukupenda!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nichukue twende nawe, na tufanye haraka! Mfalme na anilete ndani ya vyumba vyake. Tunakushangilia na kukufurahia, tutasifu upendo wako kuliko divai. Tazama jinsi ilivyo bora wakupende!
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nivute nyuma yako, na tukimbie; Mfalme ameniingiza vyumbani mwake. Tutafurahi na kukushangilia; Tutazinena pambaja zako kuliko divai; Ndiyo, ina haki wakupende.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nichukue, twende zetu haraka, mfalme amenileta katika chumba chake. Tutafurahi na kushangilia kwa sababu yako, tutasifu mapenzi yako kuliko divai. Wanawake wana haki kukupenda!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nichukue twende nawe, na tufanye haraka! Mfalme na anilete ndani ya vyumba vyake. Tunakushangilia na kukufurahia, tutasifu upendo wako zaidi kuliko divai. Tazama ni jinsi gani ilivyo haki wakupende!
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nichukue twende nawe, na tufanye haraka! Mfalme na anilete ndani ya vyumba vyake. Tunakushangilia na kukufurahia, tutasifu upendo wako zaidi kuliko divai. Tazama jinsi ilivyo bora wakupende!
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nivute nyuma yako, na tukimbie; Mfalme ameniingiza vyumbani mwake. Tutafurahi na kukushangilia; Tutalinena pendo lako kuliko divai; Ndiyo, ina haki wakupende.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nichukue, twende zetu haraka, mfalme amenileta katika chumba chake. Tutafurahi na kushangilia kwa sababu yako, tutasifu mapenzi yako kuliko divai. Wanawake wana haki kukupenda!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nivute, nikufuate nyuma! Na tupige mbio! Hata mfalme akiniingiza vijumbani mwake, na tupige vigelegele kwa kukufurahia wewe! Huo upendo wako tuutukuze kuliko mvinyo! Wanakupenda kwelikweli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nivute nyuma yako, na tukimbie; Mfalme ameniingiza vyumbani mwake. Tutafurahi na kukushangilia; Tutazinena pambaja zako kuliko divai; Ndiyo, ina haki wakupende.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Unipeleke, tuende haraka, mufalme amenileta katika chumba chake. Tutafurahi na kukushangilia pamoja, tutasifu mapenzi yako kuliko divai. Wabinti wana haki ya kukupenda!