Song of Solomon 3:10 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nguzo zake zilitengenezwa kwa fedha; mgongo wake kwa dhahabu; mahali pa kukalia pamefunikwa vitambaa vya zambarau, walichoshona kwa upendo wanawake wa Yerusalemu, waliokishonea alama za upendo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nguzo zake alizitengeneza kwa fedha, kitako chake kwa dhahabu. Kiti chake kilipambwa kwa zambarau, gari lake likanakshiwa njumu kwa upendo na binti za Yerusalemu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nguzo zake alizifanyiza za fedha, Na mgongo wake wa dhahabu, Kiti chake kimepambwa urujuani, Gari lake limenakishiwa njumu, Hiba ya binti za Yerusalemu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nguzo zake zilitengenezwa kwa fedha; mgongo wake kwa dhahabu; mahali pa kukalia pamefunikwa vitambaa vya zambarau, walichoshona kwa upendo wanawake wa Yerusalemu. waliokishonea alama za upendo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nguzo zake alitengeneza za fedha, kitako chake kwa dhahabu. Kiti chake kilikuwa kimepambwa kwa zambarau, gari lake limenakishiwa njumu, kwa ndani limefunikwa kwa upendo wa binti za Yerusalemu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nguzo zake alizitengeneza kwa fedha, kitako chake kwa dhahabu. Kiti chake kilipambwa kwa zambarau, gari lake likanakshiwa njumu kwa upendo na binti za Yerusalemu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nguzo zake alizitengeneza za fedha, Na mgongo wake wa dhahabu, Kiti chake kimepambwa urujuani, Gari lake limenakishiwa njumu, Hiba ya binti za Yerusalemu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nguzo zake zilitengenezwa kwa fedha; mgongo wake kwa dhahabu; mahali pa kukalia pamefunikwa vitambaa vya zambarau, walichoshona kwa upendo wanawake wa Yerusalemu, waliokishonea alama za upendo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
miguu yake aliifanya kwa fedha, maegemeo ni ya dhahabu, pa kukalia ni nguo nyekundu za kifalme. Hapo kati yako marembo mazuri mno yaliyoshonwa na wanawake wa Yerusalemu ya kumpendeza mfalme.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nguzo zake alizifanyiza za fedha, Na mgongo wake wa dhahabu, Kiti chake kimepambwa urujuani, Gari lake limenakishiwa njumu, Hiba ya binti za Yerusalemu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nguzo zake zilitengenezwa kwa feza, nafasi ya kuegemea imefunikwa kwa zahabu, nafasi ya kuikalia imefunikwa na vitambaa vya nyekundu-nyeusi. Katikati yake kilipambwa na wabinti wa Yerusalema waliokishonea vitambulisho vya upendo.