Song of Solomon 4:10 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Dada yangu, bi arusi; pendo lako ni tamu ajabu. Ni bora kuliko divai, marashi yako yanukia kuliko viungo vyote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Tazama jinsi pendo lako linavyofurahisha, dada yangu, bibi arusi wangu! Pendo lako linafurahisha aje zaidi ya divai, na harufu ya marhamu yako zaidi ya manukato yoyote!
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Jinsi zilivyo nzuri pambaja zako, umbu langu, Bibi arusi, ni nzuri kupita divai; Na harufu ya marhamu yako Yapita manukato ya kila namna.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Dada yangu, bi arusi; pendo lako ni tamu ajabu. Ni bora kuliko divai, marashi yako yanukia kuliko viungo vyote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Tazama jinsi pendo lako linavyofurahisha, dada yangu, bibi arusi wangu! Ni mara ngapi zaidi pendo lako linafurahisha kuliko divai, na harufu ya manukato yako zaidi kuliko kikolezo cho chote!
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Tazama jinsi pendo lako linavyofurahisha, dada yangu, bibi arusi wangu! Pendo lako linafurahisha aje zaidi ya divai, na harufu ya manukato yako zaidi ya kikolezo chochote!
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Jinsi pendo lako lilivyo zuri, dada yangu, Bibi harusi, ni mzuri kupita divai; Na harufu ya marhamu yako Yapita manukato ya kila namna.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Dada yangu, bi arusi; pendo lako ni tamu ajabu. Ni bora kuliko divai, marashi yako yanukia kuliko viungo vyote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ni kuzuri mno kukumbatiana na wewe, uliye umbu langu na mchumba wangu; kukumbatiana na wewe kunapendeza kuliko kunywa mvinyo, mnuko wa mafuta yako ni mzuri kuliko wa manukato yote.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Jinsi zilivyo nzuri pambaja zako, umbu langu, Bibi arusi, ni nzuri kupita divai; Na harufu ya marhamu yako Yapita manukato ya kila namna.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Dada yangu, muchumba wangu; mapendo yako yananivuta ajabu. Ni bora kuliko divai, marasi yako yananuka vizuri kuliko viungo vyote.