Song of Solomon 4:11 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Midomo yako yadondosha asali, ee bibiarusi wangu; ulimi wako una asali na maziwa. Harufu nzuri ya mavazi yako ni kama ya Lebanoni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Midomo yako inadondosha utamu kama sega la asali, bibi arusi wangu; maziwa na asali viko chini ya ulimi wako. Harufu nzuri ya mavazi yako ni kama ile ya Lebanoni.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bibi arusi, midomo yako yadondoza asali, Asali na maziwa vi chini ya ulimi wako; Na harufu ya mavazi yako Ni kama harufu ya Lebanoni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Midomo yako yadondosha asali, ee bibiarusi wangu; ulimi wako una asali na maziwa. Harufu nzuri ya mavazi yako ni kama ya Lebanoni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Midomo yako inadondosha utamu kama sega la asali, bibi arusi wangu; maziwa na asali viko chini ya ulimi wako. Harufu nzuri ya mavazi yako ni kama ile ya Lebanoni.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Midomo yako inadondosha utamu kama sega la asali, bibi arusi wangu; maziwa na asali viko chini ya ulimi wako. Harufu nzuri ya mavazi yako ni kama ile ya Lebanoni.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Bibi harusi, midomo yako yadondosha asali, Asali na maziwa viko chini ya ulimi wako; Na harufu ya mavazi yako Ni kama harufu ya Lebanoni.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Midomo yako yadondosha asali, ee bibiarusi wangu; ulimi wako una asali na maziwa. Harufu nzuri ya mavazi yako ni kama ya Lebanoni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Midomo yako, mchumba wangu, inadondoka asali safi, asali na maziwa ndiyo yaliyoko chini ya ulimi wako, nao mnuko wa mavazi yako ni mzuri kama wa Libanoni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Bibi arusi, midomo yako yadondoza asali, Asali na maziwa vi chini ya ulimi wako; Na harufu ya mavazi yako Ni kama harufu ya Lebanoni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Midomo yako inadondosha asali, ee muchumba wangu, ulimi wako una asali na maziwa. Harufu nzuri ya nguo zako ni kama miti ya Lebanoni.