Song of Solomon 5:1 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Naingia bustanini mwangu, dada yangu, bi arusi. Nakusanya manemane na viungo, nala sega langu la asali, nanywa divai yangu na maziwa yangu. Kuleni enyi marafiki, kunyweni; kunyweni sana wapendwa wangu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nimekuja kwenye bustani yangu, dada yangu, bibi arusi wangu; nimekusanya manemane yangu pamoja na manukato yangu. Nimekula sega langu la asali na asali yangu; nimekunywa divai yangu na maziwa yangu. Kuleni, enyi rafiki, mnywe; kunyweni ya kutosha, ee wapenzi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naingia bustanini mwangu, umbu langu, bibi arusi, Nachuma manemane yangu na rihani, Nala sega la asali na asali yangu, Nanywa divai yangu na maziwa. Kaleni, rafiki zangu, kanyweni, Naam, nyweni sana, wapendwa wangu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Naingia bustanini mwangu, dada yangu, bi arusi. Nakusanya manemane na viungo, nala sega langu la asali, nanywa divai yangu na maziwa yangu. Kuleni enyi marafiki, kunyweni; kunyweni sana wapendwa wangu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nimekuja kwenye bustani yangu, dada yangu, bibi arusi wangu; nimekusanya manemane yangu pamoja na kikolezo changu. Nimekula sega langu la asali na asali yangu; nimekunywa divai yangu na maziwa yangu. Kuleni, enyi marafiki, mnywe; kunyweni ya kutosha, Ee wapenzi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nimekuja kwenye bustani yangu, dada yangu, bibi arusi wangu; nimekusanya manemane yangu pamoja na kikolezo changu. Nimekula sega langu la asali na asali yangu; nimekunywa divai yangu na maziwa yangu. Kuleni, enyi marafiki, mnywe; kunyweni ya kutosha, ee wapenzi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naingia bustanini mwangu, dada yangu, bibi harusi, Nachuma manemane yangu na rihani, Nala sega la asali na asali yangu, Nanywa divai yangu na maziwa. Kaleni, rafiki zangu, kanyweni, Naam, nyweni sana, wapendwa wangu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Naingia bustanini mwangu, dada yangu, bi arusi. Nakusanya manemane na viungo, nala sega langu la asali, nanywa divai yangu na maziwa yangu. Kuleni enyi marafiki, kunyweni; kunyweni sana wapendwa wangu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
“Ninaingia bustanini pangu, umbu langu na mchumba wangu, niunge manemane na manukato yangu, nile masega yangu pamoja na asali yangu, ninywe mvinyo yangu na maziwa yangu. Nanyi wenzangu, leni, nyweni, mpaka mleweshwe na upendo!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naingia bustanini mwangu, umbu langu, bibi arusi, Nachuma manemane yangu na rihani, Nala sega la asali na asali yangu, Nanywa divai yangu na maziwa. Kaleni, rafiki zangu, kanyweni, Naam, nyweni sana, wapendwa wangu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ninaingia katika bustani yangu, dada yangu, muchumba wangu. Ninakusanya manemane na majani yenye harufu, ninakula sega langu la asali, ninakunywa divai yangu na maziwa yangu. Mukule, enyi warafiki, mukunywe; mukunywe sana, wapendwa wangu.