Song of Solomon 5:13 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mashavu yake ni kama matuta ya rihani kama bustani iliyojaa manukato na manemane. Midomo yake ni kama yungiyungi, imelowa manemane kwa wingi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mashavu yake ni kama matuta ya mimea ya manukato. Midomo yake ni kama yungiyungi inayodondosha manemane.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mashavu yake ni kama matuta ya rihani, Ambayo hufanyizwa manukato; Midomo yake ni kama nyinyoro, Inadondoza matone ya manemane;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mashavu yake ni kama matuta ya rihani kama bustani iliyojaa manukato na manemane. Midomo yake ni kama yungiyungi, imelowa manemane kwa wingi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mashavu yake ni kama matuta ya vikolezo yakitoa manukato. Midomo yake ni kama yungiyungi inayodondosha manemane.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mashavu yake ni kama matuta ya vikolezo yakitoa manukato. Midomo yake ni kama yungiyungi inayodondosha manemane.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mashavu yake ni kama matuta ya rihani Ambayo hufanyizwa manukato; Midomo yake ni kama nyinyoro, Inadondosha matone ya manemane;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mashavu yake ni kama matuta ya rihani kama bustani iliyojaa manukato na manemane. Midomo yake ni kama yungiyungi, imelowa manemane kwa wingi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mashavu yake ni kama matuta yaliyopandwa manukato, namo juu mna vijanijani vinukavyo vizuri; midomo yake ni nyinyoro zidondokazo manemane ya majimaji.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mashavu yake ni kama matuta ya rihani, Ambayo hufanyizwa manukato; Midomo yake ni kama nyinyoro, Inadondoza matone ya manemane;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mashavu yake ni kama bustani inayojaa marasi, yenye harufu nzuri. Midomo yake ni kama yungiyungi, inatonatona manemane kwa wingi.