Song of Solomon 5:2 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nililala, lakini moyo wangu haukulala. Sauti ya mpenzi wangu anabisha hodi. “Nifungulie, dada yangu mpenzi wangu, bibiarusi wangu, hua wangu, usiye na kasoro. Kichwa changu kimelowa umande na nywele zangu manyunyu ya usiku.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nililala lakini moyo wangu ulikuwa macho. Sikiliza! Mpenzi wangu anabisha: “Nifungulie, dada yangu, mpendwa wangu, hua wangu, usiye na hitilafu. Kichwa changu kimeloa umande, na nywele zangu manyunyu ya usiku.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nalikuwa nimelala, lakini moyo wangu u macho, Sikiliza! Mpendwa wangu anabisha! Nifungulie, umbu langu, mpenzi wangu, Hua wangu, mkamilifu wangu, Kwa maana kichwa changu kimelowa umande, Nywele zangu zina manyunyu ya usiku.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nililala, lakini moyo wangu haukulala. Sauti ya mpenzi wangu anabisha hodi. “Nifungulie, dada yangu mpenzi wangu, bibiarusi wangu, hua wangu, usiye na kasoro. Kichwa changu kimelowa umande na nywele zangu manyunyu ya usiku.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nililala lakini moyo wangu ulikuwa macho. Sikiliza! Mpenzi wangu anabisha: “Nifungulie, dada yangu, mpenzi wangu, hua wangu, asiye na hitilafu. Kichwa changu kimeloa umande, na nywele zangu manyunyu ya usiku.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nililala lakini moyo wangu ulikuwa macho. Sikiliza! Mpenzi wangu anabisha: “Nifungulie, dada yangu, mpenzi wangu, hua wangu, asiye na hitilafu. Kichwa changu kimeloa umande, na nywele zangu manyunyu ya usiku.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nilikuwa nimelala, lakini moyo wangu uko macho, Sikiliza! Mpendwa wangu anabisha! Nifungulie, dada yangu, mpenzi wangu, Hua wangu, mkamilifu wangu, Kwa maana kichwa changu kimelowa umande, Nywele zangu zina manyunyu ya usiku.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nililala, lakini moyo wangu haukulala. Sauti ya mpenzi wangu anabisha hodi. “Nifungulie, dada yangu mpenzi wangu, bibiarusi wangu, hua wangu, usiye na kasoro. Kichwa changu kimelowa umande na nywele zangu manyunyu ya usiku.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nililala usingizi, lakini moyo ulikuwa macho; mara nikasikia, mpendwa wangu akigonga mlango: “Nifungulie, umbu langu, mpenzi wangu, hua yangu, mwenzangu atakataye! Kwa kuwa nimejazwa umande kichwani pangu, kwa kuwa misuko ya nywele zangu imejaa unyevu wa usiku.”
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nalikuwa nimelala, lakini moyo wangu u macho, Sikiliza! Mpendwa wangu anabisha! Nifungulie, umbu langu, mpenzi wangu, Hua wangu, mkamilifu wangu, Kwa maana kichwa changu kimelowa umande, Nywele zangu zina manyunyu ya usiku.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nililala usingizi, lakini moyo wangu ulikesha. Nikasikia mupenzi wangu akipiga hodi. Unifungulie dada, ee mupenzi wangu, muchumba wangu, njiwa yangu, usiyekuwa na kilema chochote. Kichwa changu kimelowana na umande na nywele zangu na manyunyu ya usiku.