Song of Solomon 6:11 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nimeingia katika bustani ya milozi kutazama machipuko ya bondeni, kuona kama mizabibu imechanua, na mikomamanga imechanua maua.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Niliteremka kwenye bustani ya miti ya milozi ili kutazama machipuko ya bondeni, kuona kama mizabibu imechipua au kama mikomamanga imechanua maua.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nalishukia bustani ya milozi, Ili kuyatazama machipuko ya bondeni; Nione kama mzabibu umechanua, Kama mikomamanga imetoa maua.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nimeingia katika bustani ya milozi kutazama machipuko ya bondeni, kuona kama mizabibu imechanua, na mikomamanga imechanua maua.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nilitelemka kwenye kichaka cha miti ya milozi ili kutazama machipuko ya bondeni, kuona kama mizabibu imechipua au kama mikomamanga imechanua maua.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Niliteremka kwenye bustani ya miti ya milozi ili kutazama machipuko ya bondeni, kuona kama mizabibu imechipua au kama mikomamanga imechanua maua.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nilishukia katika bustani ya milozi, Ili kuyatazama machipuko ya bondeni; Nione kama mzabibu umechanua, Kama mikomamanga imetoa maua.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nimeingia katika bustani ya milozi kutazama machipuko ya bondeni, kuona kama mizabibu imechanua, na mikomamanga imechanua maua.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nilishuka kwenda bustanini penye milozi, nijifurahishe kwa kuyaona machipukizi mapya yaliyoko bondeni; tena nilitaka kuitazama mizabibu, kama imechanua, nayo mikomamanga, kama imepata maua.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nalishukia bustani ya milozi, Ili kuyatazama machipuko ya bondeni; Nione kama mzabibu umechanua, Kama mikomamanga imetoa maua.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nimeingia katika bustani ya miti ya lozi, kuangalia vichipukizi katika bonde, kuona kama mizabibu imechanua, na mikomamanga imechanua maua.