Song of Solomon 7:12 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Tutaamka mapema, twende kwenye mashamba ya mizabibu, tukaone kama imeanza kuchipua, na kama maua ya zabibu yamekwisha kuchanua, pia kama mikomamanga imeanza kutoa maua. Huko ndiko nitakapokupatia pendo langu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hebu na twende mapema katika mashamba ya mizabibu tuone kama mizabibu imechipua, kama maua yake yamefunguka, na kama mikomamanga imetoa maua: huko nitakupa penzi langu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Twende mapema hata mashamba ya mizabibu, Tuone kama mzabihu umechanua, Na maua yake yamefunuka; Kama mikomamanga imetoa maua; Huko nitakupa pambaja zangu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Tutaamka mapema, twende kwenye mashamba ya mizabibu, tukaone kama imeanza kuchipua, na kama maua ya zabibu yamekwisha kuchanua, pia kama mikomamanga imeanza kutoa maua. Huko ndiko nitakapokupatia pendo langu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hebu na twende mapema katika mashamba ya mizabibu tuone kama mizabibu imechipua, kama maua yake yamefunguka, pia kama mikomamanga imetoa maua: huko nitakupa penzi langu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hebu na twende mapema katika mashamba ya mizabibu tuone kama mizabibu imechipua, kama maua yake yamefunguka, na kama mikomamanga imetoa maua: huko nitakupa penzi langu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Twende mapema hadi kwenye mashamba ya mizabibu, Tuone kama mzabibu umechanua, Na maua yake yamefunuka; Kama mikomamanga imetoa maua; Huko nitakupa upendo wangu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Tutaamka mapema, twende kwenye mashamba ya mizabibu, tukaone kama imeanza kuchipua, na kama maua ya zabibu yamekwisha kuchanua, pia kama mikomamanga imeanza kutoa maua. Huko ndiko nitakapokupatia pendo langu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Na tuondoke mapema kwenda mizabibuni, tutazame, kama mizabibu inachanua na kuyafunua maua. tutazama nayo mikomamanga, kama imepata maua! Hapo ndipo, nitakapokupa kukumbatiana na mimi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Twende mapema hata mashamba ya mizabibu, Tuone kama mzabihu umechanua, Na maua yake yamefunuka; Kama mikomamanga imetoa maua; Huko nitakupa pambaja zangu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kuja, ewe mupenzi wangu, tuende katika mashamba, tuende tulale kule katika vijiji.