Titus 1:12 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hata mmoja wa manabii wao, ambaye naye pia ni Mkrete, alisema: “Wakrete husema uongo daima; ni kama wanyama wabaya, walafi na wavivu!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hata mmoja wa manabii wao mwenyewe amesema, “Wakrete ni waongo siku zote, wanyama wabaya, walafi, wavivu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mtu wa kwao, nabii wao wenyewe, amesema, Wakrete ni waongo siku zote, hayawani wabaya, walafi wavivu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mmoja miongoni mwa watu wa kwao, Nabii kutoka Krete, alisema: “Wakrete ni waongo daima. Si bora kuliko wanyama wa porini. Daima wapo tayari kula, lakini hawapendi kufanya kazi.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hata mmoja wa manabii wao, ambaye naye pia ni Mkrete, alisema: “Wakrete, husema uongo daima; ni kama wanyama wabaya, walafi na wavivu!”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hata mmoja wa manabii wao, ambaye naye pia ni Mkrete, alisema: “Wakrete husema uongo daima; ni kama wanyama wabaya, walafi na wavivu!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hata mmojawapo wa manabii wao mwenyewe amesema “Wakrete ni waongo siku zote, wanyama wabaya, walafi, wavivu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hata mmojawapo wa manabii wao mwenyewe amesema, “Wakrete ni waongo siku zote, wanyama wabaya, walafi, wavivu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mmoja wao, nabii wao wenyewe, amesema, Wakrete ni waongo siku zote, wanyama wabaya, walafi wavivu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hata mmoja wa manabii wao, ambaye naye pia ni Mkrete, alisema: “Wakrete husema uongo daima; ni kama wanyama wabaya, walafi na wavivu!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mfumbuaji wa kwao aliyekuwa mwenzao wenyewe alisema: Wakreta ndio waongo kabisa, ni nyama waovu, ni matumbo mavivu;
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mtu wa kwao, nabii wao wenyewe, amesema, Wakrete ni waongo siku zote, hayawani wabaya, walafi wavivu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na hata mumoja wa manabii wao wenyewe, Mukrete, alisema: “Wakrete ni wasema uongo siku zote, nyama wabaya, wavivu na walafi.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Mtu wa kwao, nabii wao wenyewe, amesema. Wakrete ni wawongo siku zote, nyama mwitu wahaya, walafi, wasiofanya kazi. Ushuhuda huu ni kweli.