Titus 1:15 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kila kitu ni safi kwa watu walio safi; lakini hakuna chochote kilicho safi kwa wale waliochafuliwa na wasioamini, maana dhamiri na akili zao zimechafuliwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa wale walio safi, kila kitu ni safi kwao. Lakini kwa wale waliopotoka na wasioamini, hakuna chochote kilicho safi. Kwa kweli nia zao na dhamiri zao zimepotoka.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Vitu vyote ni safi kwa hao walio safi; lakini hakuna kilicho safi kwao walio wanajisi, wasioamini; bali akili zao zimekuwa najisi, na nia zao pia.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kwa wale watu wenye mawazo yaliyo safi, kila kitu ni safi. Lakini hakuna kinachoweza kuwa safi kwa wasioamini ambao dhambi zao zimewafanya kuwa wachafu. Mawazo yao daima huwa yasiyo haki, na dhamiri zao pia zimekuwa chafu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kila kitu ni safi kwa watu walio safi; lakini hakuna chochote kilicho safi kwa wale waliochafuliwa na wasioamini, maana dhamiri na akili zao zimechafuliwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kila kitu ni safi kwa watu walio safi; lakini hakuna chochote kilicho safi kwa wale waliochafuliwa na wasioamini, maana dhamiri na akili zao zimechafuliwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa wale walio safi, kila kitu ni safi kwao. Lakini kwa wale waliopotoka na wasioamini, hakuna cho chote kilicho safi. Kwa kweli nia zao na dhamiri zao zimepotoka.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa wale walio safi, kila kitu ni safi kwao. Lakini kwa wale waliopotoka na wasioamini, hakuna chochote kilicho safi. Kwa kweli nia zao na dhamiri zao zimepotoka.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Vitu vyote ni safi kwa hao walio safi; lakini hakuna kilicho safi kwao walio najisi, wasioamini; bali akili zao zimekuwa najisi, na nia zao pia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kila kitu ni safi kwa watu walio safi; lakini hakuna chochote kilicho safi kwa wale waliochafuliwa na wasioamini, maana dhamiri na akili zao zimechafuliwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wenye kutakata mioyo, vyote huwatakatia; lakini wenye mioyo michafu wasiomtegemea Mungu hakuna kiwatakiacho, maana hata mawazo yao ni machafu, mioyo isijue tena yatakatayo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Vitu vyote ni safi kwa hao walio safi; lakini hakuna kilicho safi kwao walio wanajisi, wasioamini; bali akili zao zimekuwa najisi, na nia zao pia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kila kitu ni safi kwa watu wanaokuwa safi. Lakini hakuna chochote kinachokuwa safi kwa watu wachafu na wasiomwamini Mungu, kwa maana akili na zamiri zao zimekuwa chafu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Vitu vyote ni sali kwao walio safi: lakini hapana kilicho safi kwa walio najis, wasioamini, bali akili zao na nia zao pia zimekuwa najis.