Titus 1:16 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu kama hao hujidai kwamba wanamjua Mungu, lakini kwa matendo yao humkana. Ni watu wa kuchukiza mno na wakaidi, hawafai kwa jambo lolote jema.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wanadai kumjua Mungu, lakini kwa matendo yao wanamkana. Hao watu ni chukizo, wasiotii, wasiofaa kwa jambo lolote jema.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wanakiri ya kwamba wanamjua Mungu, bali kwa matendo yao wanamkana; ni wenye machukizo, waasi, wala kwa kila tendo jema hawafai.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hao hudai kuwa wanamjua Mungu, lakini matendo yao maovu yanaonesha kwa hakika kuwa hawamjui. Ni watu wenye kuchukiza mno na wasiotii, na hawafai kwa lo lote lililo jema.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Watu kama hao hujidai kwamba wanamjua Mungu, lakini kwa matendo yao humkana. Ni watu wa kuchukiza mno na wakaidi, hawafai kwa jambo lolote jema.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu kama hao hujidai kwamba wanamjua Mungu, lakini kwa matendo yao humkana. Ni watu wa kuchukiza mno na wakaidi, hawafai kwa jambo lolote jema.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wanadai kumjua Mungu, lakini kwa matendo yao wanamkana. Hao watu ni chukizo, wasiotii, wasiofaa kwa jambo lo lote jema.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wanadai kumjua Mungu, lakini kwa matendo yao wanamkana. Hao watu ni chukizo, wasiotii, wasiofaa kwa jambo lolote jema.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wanakiri ya kwamba wanamjua Mungu, bali kwa matendo yao wanamkana; ni wenye machukizo, waasi, wala hawafai kwa tendo lolote jema.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu kama hao hujidai kwamba wanamjua Mungu, lakini kwa matendo yao humkana. Ni watu wa kuchukiza mno na wakaidi, hawafai kwa jambo lolote jema.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Huungama kwamba: Tumemjua Mungu, lakini kwa matendo yao hakuna kuwa wake. Kwani hutapisha, kwa kuwa hawatii, hawafai kabisa kufanya kazi yo yote iliyo njema.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wanakiri ya kwamba wanamjua Mungu, bali kwa matendo yao wanamkana; ni wenye machukizo, waasi, wala kwa kila tendo jema hawafai.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wanajidai kwamba wanamujua Mungu, lakini wanamukana kwa matendo yao. Wao ni wenye machukizo, waasi hata hawafai kwa kufanya kazi yo yote nzuri.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Wanakiri kwamha wanamjua Mungu, bali kwa matendo yao wanamkana, ni wenye machukizo, maasi, na kwa killa tendo jema hawafai.