Titus 1:3 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
na wakati ufaao ulipowadia, akaudhihirisha katika ujumbe wake. Mimi nilikabidhiwa ujumbe huo niutangaze kufuatana na amri ya Mungu, Mwokozi wetu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
naye kwa wakati wake aliouweka alilidhihirisha neno lake kupitia kwa mahubiri ambayo mimi nimewekewa amana kwa amri ya Mungu Mwokozi wetu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
akalifunua neno lake kwa majira yake katika ule ujumbe niliowekewa amana mimi kwa amri ya Mwokozi wetu Mungu;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Na wakati sahihi ulipotimia aliidhihirisha ile habari njema. Ujumbe huo ulikabidhiwa kwangu kwa amri ya Mungu Mwokozi wetu kumwambia kila mtu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
na wakati ufaao ulipowadia, akaudhihirisha katika ujumbe wake. Mimi nilikabidhiwa ujumbe huo nuutangaze kufuatana na amri ya Mungu, Mwokozi wetu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
na wakati ufaao ulipowadia, akaudhihirisha katika ujumbe wake. Mimi nilikabidhiwa ujumbe huo niutangaze kufuatana na amri ya Mungu, Mwokozi wetu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
naye kwa wakati wake aliouweka alilidhihirisha neno lake kwa njia ya mahubiri ambayo mimi nimewekewa amana kwa amri ya Mungu Mwokozi wetu:
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
naye kwa wakati wake aliouweka alilidhihirisha neno lake kwa njia ya mahubiri ambayo mimi nimewekewa amana kwa amri ya Mungu Mwokozi wetu:
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
akalifunua neno lake kwa majira yake katika ule ujumbe niliokabidhiwa kwa amri ya Mwokozi wetu Mungu;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
na wakati ufaao ulipowadia, akaudhihirisha katika ujumbe wake. Mimi nilikabidhiwa ujumbe huo niutangaze kufuatana na amri ya Mungu, Mwokozi wetu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
lakini siku zake zilipotimia, akalifufua Neno lake akiitangaza mbiu, niliyopewa nami kuipiga, kama nilivyoagizwa na mwokozi wetu Mungu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
akalifunua neno lake kwa majira yake katika ule ujumbe niliowekewa amana mimi kwa amri ya Mwokozi wetu Mungu;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Alifunua neno lake kwa wakati alioupanga kwa njia ya mahubiri ambayo yeye Mungu Mwokozi wetu aliyoniamuru kutangaza.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
akalifunua neno lake kwa nyakati zake katika ule ujumbe nilioaminiwa mimi kwa amri ya Mwokozi wetu, Mungu: