Titus 1:4 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ninakuandikia wewe Tito, mwanangu wa kweli katika imani tunayoshiriki. Nakutakia neema na amani kutoka kwa Mungu Baba, na kutoka kwa Kristo Yesu, Mkombozi wetu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa Tito, mwanangu hasa katika imani tunayoshiriki sote. Neema na amani zitokazo kwa Mungu, Baba yetu, na kwa Bwana wetu Isa Al-Masihi, Mwokozi wetu, ziwe nawe.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
kwa Tito, mwanangu hasa katika imani tuishirikiyo. Neema na iwe kwako na amani zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Kristo Yesu Mwokozi wetu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Nakuandikia wewe Tito, mwanangu halisi katika imani tunayoshiriki: Neema na amani kutoka kwa Mungu Baba, na kutoka kwa Kristo Yesu Mwokozi wetu iwe nanyi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Ninakuandikia wewe Tito, mwanangu wa kweli katika imani tunayoshiriki. Nakutakia neema na amani kutoka kwa Mungu Baba, na kutoka kwa Kristo Yesu, Mkombozi wetu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ninakuandikia wewe Tito, mwanangu wa kweli katika imani tunayoshiriki. Nakutakia neema na amani kutoka kwa Mungu Baba, na kutoka kwa Kristo Yesu, Mkombozi wetu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa Tito, mwanangu hasa katika imani tunayoshiriki sote: Neema iwe kwako na amani itokayo kwa Mungu Baba na kwa Kristo Yesu Mwokozi wetu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa Tito, mwanangu hasa katika imani tunayoshiriki sote: Neema iwe kwako na amani itokayo kwa Mungu Baba na kwa Al-Masihi Isa Mwokozi wetu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
kwa Tito, mwanangu halisi katika imani tunayoshiriki. Neema na iwe kwako na amani zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Kristo Yesu Mwokozi wetu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ninakuandikia wewe Tito, mwanangu wa kweli katika imani tunayoshiriki. Nakutakia neema na amani kutoka kwa Mungu Baba, na kutoka kwa Kristo Yesu, Mkombozi wetu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nakuandikia wewe, Tito, maana u mwanangu wa kweli kwa hivyo, tulivyo mmoja kwa kumtegemea Mungu. Upole ukukalie na utengemano unaotoka kwa Mungu Baba na kwa mwokozi wetu Kristo Yesu!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
kwa Tito, mwanangu hasa katika imani tuishirikiyo. Neema na iwe kwako na amani zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Kristo Yesu Mwokozi wetu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ninakutumia barua hii, wewe Tito, mwana wangu wa kweli katika imani tunayoshiriki pamoja. Ninakutakia neema na amani kutoka kwa Mungu Baba na kwa Yesu Kristo Mwokozi wetu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
kwa Tito, mwanangu katika imani tuishirikiyo: Neema na rehema na amani zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Bwana Yesu Kristo, Mwokozi wetu.