Titus 1:5 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nilikuacha Krete ili urekebishe yale mambo ambayo hayakuwa yamekamilika bado, na kuwateua wazee wa kanisa katika kila mji. Kumbuka maagizo yangu:
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Sababu yangu ya kukuacha huko Krete ni ili uweke utaratibu mambo yale yaliyosalia na kuwateua wazee wa kundi la waumini katika kila mji, kama nilivyokuagiza.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa sababu hii nalikuacha Krete, ili uyatengeneze yaliyopunguka, na kuweka wazee katika kila mji kama vile nilivyokuamuru;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Nilikuacha kule Krete ili uweze kuyakamilisha yale yaliyokuwa yamebaki kufanyiwa kazi. Kisha nakuagiza uteue wazee na kuwaweka kuwa viongozi katika kila mji.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Nilikuacha Krete ili urekebishe yale mambo ambayo hayakuwa yamekamilika bado, na kuwateua wazee wa kanisa katika kila mji. Kumbuka maagizo yangu:
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nilikuacha Krete ili urekebishe yale mambo ambayo hayakuwa yamekamilika bado, na kuwateua wazee wa kanisa katika kila mji. Kumbuka maagizo yangu:
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Sababu ya mimi kukuacha huko Krete ni ili uweke kwenye utaratibu mambo yale yaliyosalia na kuwaweka wazee wa kanisa katika kila mji, kama nilivyokuagiza.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Sababu ya mimi kukuacha huko Krete ni ili uweke utaratibu mambo yale yaliyosalia na kuwaweka viongozi wa makundi ya waumini katika kila mji, kama nilivyokuagiza.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa sababu hii nilikuacha Krete, ili uyatengeneze yaliyopunguka, na kuwateua wazee katika kila mji kama vile nilivyokuamuru;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nilikuacha Krete ili urekebishe yale mambo ambayo hayakuwa yamekamilika bado, na kuwateua wazee wa kanisa katika kila mji. Kumbuka maagizo yangu:
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa sababu hii nilikuacha katika Kreta, uyatengeneze yaliyosalia, uiweekee miji yote wazee, kama nilivyokuagiza:
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa sababu hii nalikuacha Krete, ili uyatengeneze yaliyopunguka, na kuweka wazee katika kila mji kama vile nilivyokuamuru;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nimekuacha katika kisanga cha Krete kusudi upate kutengeneza maneno yaliyobaki na kusimika wazee katika kanisa ndani ya kila muji, ukifuata maagizo niliyokutolea:
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa sababu hii nalikuaeba katika Krete, illi nyatengeneze yaliyosalia, na kuweka wazee katika killa mji kama nilivyokuamuru;