Titus 1:6 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mzee wa kanisa anapaswa kuwa mtu asiye na hatia; aliye na mke mmoja tu, na watoto wake wanapaswa kuwa waumini, wasiojulikana kuwa wakorofi au wakaidi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mzee wa kundi la waumini asiwe na lawama, awe mume wa mke mmoja, mtu ambaye watoto wake ni waumini, wala hawashtakiwi kwa ufisadi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
ikiwa mtu hakushitakiwa neno, naye ni mume wa mke mmoja, ana watoto waaminio, wasioshitakiwa kuwa ni wafisadi wala wasiotii.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Anayeweza kuteuliwa ni yule ambaye halaumiwi kwa matendo yoyote mabaya, na aliye mwaminifu kwa mkewe, na anao watoto wanaoamini Mungu na ambao sio wakaidi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
mzee wa kanisa anapaswa kuwa mtu asiye na hatia; aliye na mke mmoja tu, na watoto wake wanapaswa kuwa waumini, wasiojulikana kuwa wakorofi au wakaidi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
mzee wa kanisa anapaswa kuwa mtu asiye na hatia; aliye na mke mmoja tu, na watoto wake wanapaswa kuwa waumini, wasiojulikana kuwa wakorofi au wakaidi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mzee wa kanisa asiwe na lawama, awe mume wa mke mmoja, mtu ambaye watoto wake ni waaminio na wala hawashtakiwi kwa ufisadi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kiongozi wa kundi la waumini asiwe na lawama, awe mume wa mke mmoja, mtu ambaye watoto wake ni waaminio na wala hawashtakiwi kwa ufisadi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
ikiwa mtu hakushitakiwa neno, naye ni mume wa mke mmoja, ana watoto waaminio, wasioshitakiwa kuwa ni wafisadi wala wasiotii.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mzee wa kanisa anapaswa kuwa mtu asiye na hatia; aliye na mke mmoja tu, na watoto wake wanapaswa kuwa waumini, wasiojulikana kuwa wakorofi au wakaidi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
akiwa mtu asiye na neno la kumkamia, aliye mume wa mke mmoja, tena mwenye watoto waelekevu wasiosingiziwa kuwa waasherati wala wabezi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
ikiwa mtu hakushitakiwa neno, naye ni mume wa mke mmoja, ana watoto waaminio, wasioshitakiwa kuwa ni wafisadi wala wasiotii.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
muzee wa kanisa anapaswa kuwa mutu asiyeshitakiwa neno lolote. Sherti akuwe na muke mumoja nao watoto wake wanapaswa kuwa waamini na wasioshitakiwa neno juu ya mwenendo mubaya au juu ya kukosa utii.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
ikiwa mtu hakushitakiwa neno, nae ni mume wa mke mmoja, ana watoto waaminio, wasioshitakiwa kuwa ni asharati na wasiotii.