Titus 1:8 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Anapaswa kuwa mkarimu na anayependa mambo mema. Anapaswa kuwa mtu mtaratibu, mwadilifu, mtakatifu na mwenye nidhamu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Bali awe mkarimu, anayependa mema, mwenye kiasi, mwenye haki, mwadilifu, mnyofu, mtakatifu na mwenye kuitawala nafsi yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
bali awe mkaribishaji, mpenda wema, mwenye kiasi, mwenye haki, mtakatifu, mwenye kudhibiti nafsi yake;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mzee anapaswa kuwa mtu anayewakaribisha watu nyumbani mwake. Anapaswa kuyapenda yaliyo mema. Azingatie kuishi maisha yaliyo matakatifu. Na awe na uwezo wa kudhibiti nafsi yake.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Anapaswa kuwa mkarimu na anayependa mambo mema. Anapaswa kuwa mtu mtaratibu, mwadilifu, mtakatifu na mwenye nidhamu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Anapaswa kuwa mkarimu na anayependa mambo mema. Anapaswa kuwa mtu mtaratibu, mwadilifu, mtakatifu na mwenye nidhamu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Bali awe mkarimu, anayependa mema, mwenye kiasi, mwenye haki, mwadilifu, mnyofu, mtakatifu na mwenye kuitawala nafsi yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Bali awe mkarimu, anayependa mema, mwenye kiasi, mwenye haki, mwadilifu, mnyofu, mtakatifu na mwenye kuitawala nafsi yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
bali awe mkarimu, mpenda wema, mwenye kiasi, mwenye haki, mtakatifu, mwenye kudhibiti nafsi yake;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Anapaswa kuwa mkarimu na anayependa mambo mema. Anapaswa kuwa mtu mtaratibu, mwadilifu, mtakatifu na mwenye nidhamu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ila sharti awe mpenda wageni na mpenda mema na mwerevu wa kweli na mwongofu na mcha Mungu na mwenye kujikataza mabaya!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
bali awe mkaribishaji, mpenda wema, mwenye kiasi, mwenye haki, mtakatifu, mwenye kudhibiti nafsi yake;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini inafaa akuwe mwenye kupenda kukaribisha wageni, mwenye kupenda mema, mukadirifu, mwenye haki, mutakatifu na mutaratibu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
bali awe mkaribishaji, mpenda wema, mwenye kiasi, mwenye haki, mtakatifu, mwenye kujimudu nafsi yake;