Titus 1:9 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ni lazima ashike kikamilifu ujumbe ule wa kuaminika kama unavyofundishwa. Ndivyo atakavyoweza kuwatia wengine moyo kwa mafundisho sahihi na kuyafichua makosa ya wale wanaoyapinga mafundisho hayo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lazima alishike kwa uthabiti lile neno la imani kama lilivyofundishwa, ili aweze kuwatia moyo wengine kwa mafundisho yenye uzima na kuwakanusha wale wanaopingana nayo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
akilishika lile neno la imani vile vile kama alivyofundishwa, apate kuweza kuwaonya watu kwa mafundisho yenye uzima, na kuwashinda wenye kupinga.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Anapaswa kuwa mwaminifu kwa ujumbe ule ule wa kweli tunaofundisha. Kwa namna hiyo ataweza kuwatia moyo wengine kwa mafundisho ya kweli na yenye manufaa. Na ataweza kuwathibitishia wale wanaopinga mafundisho yake ya kuwa hawako sahihi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Ni lazima ashike kikamilifu ujumbe ule wa kuaminika kama unavyofundishwa. Ndivyo atakavyoweza kuwatia wengine moyo kwa mafundisho ya kweli na kuyafichua makosa ya wale wanaoyapinga mafundisho hayo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ni lazima ashike kikamilifu ujumbe ule wa kuaminika kama unavyofundishwa. Ndivyo atakavyoweza kuwatia wengine moyo kwa mafundisho sahihi na kuyafichua makosa ya wale wanaoyapinga mafundisho hayo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Inampasa alishike kwa uthabiti lile neno la imani kama lilivyofundishwa, kusudi aweze kuwafundisha wengine kwa mafundisho manyofu na kuwakanusha wale wanaopingana nayo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Inampasa alishike kwa uthabiti lile neno la imani kama lilivyofundishwa, kusudi aweze kuwaonya wengine kwa mafundisho manyofu na kuwakanusha wale wanaopingana nayo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
akilishika lile neno la imani vile vile kama alivyofundishwa, apate kuweza kuwaonya watu kwa mafundisho yenye uzima, na kuwashinda wenye kupinga.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ni lazima ashike kikamilifu ujumbe ule wa kuaminika kama unavyofundishwa. Ndivyo atakavyoweza kuwatia wengine moyo kwa mafundisho sahihi na kuyafichua makosa ya wale wanaoyapinga mafundisho hayo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Sharti ashikamane na kulitegemea Neno, tulilofundishwa, maana ajue kuituliza mioyo yao wale, atakaowafundisha njia ya uzima, tena ajue kuwashinda hata wabishi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
akilishika lile neno la imani vile vile kama alivyofundishwa, apate kuweza kuwaonya watu kwa mafundisho yenye uzima, na kuwashinda wenye kupinga.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Anapaswa kushika Neno la kweli linalolingana na mafundisho yetu. Hivi ataweza kuwaonya watu kwa njia ya mafundisho ya kweli na kuwashinda wale wanaomupinga.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
alishikae neno la imani kama alivyofundishwa, apate kuweza kuwaonya watu kwa mafundisho yenye uzima, na kuwashinda wenye kupingana nae.