Titus 2:1 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini wewe unapaswa kuhubiri mafundisho sahihi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Bali wewe fundisha yale yaliyo sahihi kulingana na mafundisho ya kweli.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini wewe nena mambo yapasayo mafundisho yenye uzima;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini wewe Tito daima uwaambie waaminio mambo yanayokubaliana na mafundisho ya kweli na yenye uzima.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini wewe unapaswa kuhubiri mafundisho safi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini wewe unapaswa kuhubiri mafundisho sahihi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini kwa habari yako wewe, inakupasa kufundisha kulingana na mafundisho yenye uzima.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Inakupasa kufundisha itikadi sahihi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini wewe, nena mambo yanayoambatana na mafundisho mema;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini wewe unapaswa kuhubiri mafundisho sahihi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini wewe sema yapatanayo na ufundisho utupao uzima!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini wewe nena mambo yapasayo mafundisho yenye uzima;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini kwa ngambo yako, ufundishe maneno yale yanayolingana na mafundisho ya kweli.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
BALI wewe nena mambo yapasayo mafundisho ya uzima,