Titus 2:14 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yeye alijitoa mwenyewe kwa ajili yetu ili atukomboe kutoka katika uovu wote na kutufanya watu safi walio wake yeye mwenyewe, watu walio na hamu ya kutenda mema.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndiye alijitoa nafsi yake kwa ajili yetu, ili atukomboe kutoka uovu wote na kujisafishia watu kuwa mali yake Mwenyewe, yaani wale walio na juhudi katika kutenda mema.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili yetu, ili atukomboe na maasi yote, na kujisafishia watu wawe milki yake mwenyewe, wale walio na juhudi katika matendo mema.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Alijitoa mwenyewe kwa ajili yetu ili aweze kutuweka huru sisi kutoka katika uovu wote na kuweza kutusafisha kwa ajili yake watu walio wake mwenyewe, wale walio na shauku ya kufanya matendo mema.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yeye alijitoa mwenyewe kwa ajili yetu ili atukomboe kutoka katika uovu wote na kutufanya watu safi walio wake yeye mwenyewe, watu walio na hamu ya kutenda mema.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yeye alijitoa mwenyewe kwa ajili yetu ili atukomboe kutoka katika uovu wote na kutufanya watu safi walio wake yeye mwenyewe, watu walio na hamu ya kutenda mema.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
yeye ndiye aliyejitoa nafsi yake kwa ajili yetu ili atukomboe kutoka katika uovu wote na kujisafishia watu kuwa mali yake Mwenyewe, yaani, wale walio na bidii katika kutenda mema.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndiye alijitoa nafsi yake kwa ajili yetu, ili atukomboe kutoka uovu wote na kujisafishia watu kuwa mali yake Mwenyewe, yaani, wale walio na juhudi katika kutenda mema.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili yetu, ili atukomboe na maasi yote, na kujisafishia watu wake mwenyewe walio na bidii katika matendo mema.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yeye alijitoa mwenyewe kwa ajili yetu ili atukomboe kutoka katika uovu wote na kutufanya watu safi walio wake yeye mwenyewe, watu walio na hamu ya kutenda mema.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yeye ndiye aliyejitoa mwenyewe kwa ajili yetu kuwa kole ya kuyalipa mapotovu yote, ajipatie watu wang'avu watakaokuwa wake wenye bidii ya kufanya kazi nzuri.*
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili yetu, ili atukomboe na maasi yote, na kujisafishia watu wawe milki yake mwenyewe, wale walio na juhudi katika matendo mema.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yeye alijitoa mwenyewe kwa ajili yetu, kusudi atukomboe toka uovu wote na kututakasa tupate kuwa watu wake wa pekee, watu wanaokuwa na hamu ya kufanya kazi nzuri.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
aliyejitoa nafsi yake kwa ajili yetu, illi atuokoe na maasi yote, na kujisafishia watu wawe milki yake, walio na juhudi kwa matendo mema.