Titus 2:15 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, sema mambo hayo na tumia mamlaka yako yote ukiwahimiza na kuwaonya wasikilizaji wako. Mtu yeyote na asikudharau.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi wewe fundisha mambo haya. Himiza na kukaripia kwa mamlaka yote. Usiruhusu mtu yeyote akudharau.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nena maneno hayo, onya na kukaripia kwa mamlaka yote; asikudharau mtu awaye yote.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Endelea kufundisha ukihimiza na kukemea kuhusu mambo haya, na fanya hivyo kwa mamlaka yote, na mtu yeyote asikudharau.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, fundisha mambo hayo na tumia mamlaka yako yote ukiwahimiza na kuwaonya wasikilizaji wako. Mtu yeyote na asikudharau.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, sema mambo hayo na tumia mamlaka yako yote ukiwahimiza na kuwaonya wasikilizaji wako. Mtu yeyote na asikudharau.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi wewe fundisha mambo haya; onya na karipia kwa mamlaka yote. Mtu ye yote asikudharau.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi wewe fundisha mambo haya. Onya na kukaripia kwa mamlaka yote. Mtu yeyote asikudharau.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nena mambo hayo, onya na kukaripia kwa mamlaka yote; asikudharau mtu awaye yote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, sema mambo hayo na tumia mamlaka yako yote ukiwahimiza na kuwaonya wasikilizaji wako. Mtu yeyote na asikudharau.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hayo yaseme na kuwaonya na kuwashinda wakosaji kwa nguvu zote! Mtu asikubeze
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nena maneno hayo, onya na kukaripia kwa mamlaka yote; asikudharau mtu awaye yote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Haya ndiyo maneno unayopaswa kufundisha, ukiwaonya watu na kuwakaripia kwa mamlaka yote. Usijiachilie kuzarauliwa na mutu yeyote.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nena maneno hayo, ukaonye ukakaripie kwa mamlaka yote; mtu aliye yote asikudharau.