Titus 2:7 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Katika mambo yote wewe mwenyewe unapaswa kuwa mfano wa matendo mema. Uwe mnyofu na uwe na uzito katika mafundisho yako.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Katika kila jambo uwe kielelezo kwa kutenda mema. Katika mafundisho yako uoneshe uadilifu, utaratibu,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
katika mambo yote ukijionyesha wewe mwenyewe kuwa kielelezo cha matendo mema, na katika mafundisho yako ukionyesha usahihi na ustahivu,
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Katika kila kitu ujioneshe kuwa wewe ni mfano wa matendo mema. Katika mafundisho yako onesha kuwa una moyo safi na uko makini.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Katika mambo yote wewe mwenyewe unapaswa kuwa mfano wa matendo mema. Uwe mnyofu na uwe na uzito katika mafundisho yako.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Katika mambo yote wewe mwenyewe unapaswa kuwa mfano wa matendo mema. Uwe mnyofu na uwe na uzito katika mafundisho yako.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Katika kila jambo wewe mwenyewe uwe kielelezo cha matendo mema na katika mafundisho yako uonyeshe unyofu, utaratibu, ukweli
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Katika kila jambo uwe kielelezo kwa kutenda mema. Katika mafundisho yako uonyeshe uadilifu, utaratibu,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
katika mambo yote ukijionesha wewe mwenyewe kuwa kielelezo cha matendo mema, na katika mafundisho yako ukionesha usahihi na ustahivu,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Katika mambo yote wewe mwenyewe unapaswa kuwa mfano wa matendo mema. Uwe mnyofu na uwe na uzito katika mafundisho yako.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Katika mambo yote ujiweke mwenyewe kuwawia kielezo cha kujifundishia matendo mazuri! Wafundishe kujiangalia miili, waipe macheo yaipasayo!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
katika mambo yote ukijionyesha wewe mwenyewe kuwa kielelezo cha matendo mema, na katika mafundisho yako ukionyesha usahihi na ustahivu,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na wewe unapaswa kuwa mufano katika matendo mema, ukionyesha ukweli na heshima katika mafundisho yako.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
katika mambo yote ukijionyesha kuwa namna ya matendo mema, katika mafundisho yako ukionyesha usahihi na ustahifu,