Titus 2:8 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maneno yako yasiwe na hitilafu yoyote ili maadui zako waaibike wasipopata chochote kibaya cha kusema juu yetu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
na usemi sahihi usio na lawama, ili wanaokupinga watahayari, wakose neno lolote baya la kusema kutuhusu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
na maneno yenye uzima yasiyoweza kuhukumiwa makosa, ili yule mwenye kupinga atahayarike, kwa kuwa hana neno baya la kunena juu yetu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ufundishe kile ambacho ni sahihi kwa wazi, ili asiwepo yeyote atakayepinga mafundisho yako. Tumia mazuri ambayo hayatasemwa vibaya ili wale wanaokupinga waaibishwe kwa ajili ya kukosa lo lote baya la kusema dhidi yetu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Maneno yako yasiwe na hitilafu yoyote ili adui zako waaibike wasipopata chochote kibaya cha kusema juu yetu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maneno yako yasiwe na hitilafu yoyote ili maadui zako waaibike wasipopata chochote kibaya cha kusema juu yetu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
na maneno yenye uzima, yale ambayo hayawezi kulaumiwa, hata wale wenye kukupinga watahayari, wakose neno lo lote baya la kusema juu yetu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
na usemi sahihi usio na lawama, ili wanaokupinga watahayari, wakose neno lolote baya la kusema juu yetu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
na maneno yafaayo yasiyoweza kuhukumiwa makosa, ili yule mwenye kupinga atahayarike, kwa kuwa hana neno baya la kunena juu yetu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maneno yako yasiwe na hitilafu yoyote ili maadui zako waaibike wasipopata chochote kibaya cha kusema juu yetu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Litangaze Neno litupalo uzima lisilobishika, mpingani aingiwe na soni, asiweze kusema neno ovu lo lote la kutusuta!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
na maneno yenye uzima yasiyoweza kuhukumiwa makosa, ili yule mwenye kupinga atahayarike, kwa kuwa hana neno baya la kunena juu yetu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ufundishe maneno ya kweli watu wasiyoweza kubishia, hata wale wanaokupinga wapate haya kwa kukosewa na neno baya la kusema juu yetu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
na maneno yenye uzima yasiyoweza kuhukumiwa, illi yule mwenye kupingana nawe ataliayarike, kwa kuwa hana neno baya la kunena juu yetu.