Titus 3:14 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ni lazima watu wetu wajifunze kuutumia wakati wao katika kutenda mema ili wasaidie katika mahitaji ya kweli, na maisha yao yawe ya kufaa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Watu wetu hawana budi kujifunza kutenda mema, ili waweze kuyakimu mahitaji ya kila siku, wasije wakaishi maisha yasiyokuwa na matunda.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Watu wetu nao wajifunze kudumu katika matendo mema, kwa matumizi yaliyo lazima, ili wasiwe hawana matunda.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Watu wetu wanapaswa kujifunza kujihusisha katika kutenda mema ili kusaidia kukitokea mahitaji, ili wasiwe watu wasiokuwa na manufaa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Ni lazima watu wetu wajifunze kuutumia wakati wao katika kutenda mema ili wasaidie katika mahitaji ya kweli, na maisha yao yawe ya kufaa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ni lazima watu wetu wajifunze kuutumia wakati wao katika kutenda mema ili wasaidie katika mahitaji ya kweli, na maisha yao yawe ya kufaa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Watu wetu hawana budi kujifunza kujitoa kutenda mema, ili waweze kuwasaidia watu wenye mahitaji ya lazima ya kila siku, wasije wakaishi maisha yasiyokuwa na matunda.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Watu wetu hawana budi kujifunza kutenda mema, ili waweze kuyakimu mahitaji ya kila siku, wasije wakaishi maisha yasiyokuwa na matunda.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Watu wetu nao wajifunze kudumu katika matendo mema, kwa matumizi yaliyo lazima, ili wasiwe hawana matunda.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ni lazima watu wetu wajifunze kuutumia wakati wao katika kutenda mema ili wasaidie katika mahitaji ya kweli, na maisha yao yawe ya kufaa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hapo wa kwetu nao wajifunze kufanya kazi zilizo nzuri kuliko za wengine! Ikiwa wanatakwa, na wapatie wengine yatakayowatunza, wasifanane na miti isiyozaa!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Watu wetu nao wajifunze kudumu katika matendo mema, kwa matumizi yaliyo lazima, ili wasiwe hawana matunda.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Inafaa watu wetu vilevile wajifunze kuzidi kutenda mema kusudi wapate kutoa musaada kwa ajili ya mahitaji ya kweli. Na hivi maisha yao yatakuwa yenye mafaa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Watu wetu nao wajifunze kudumu katika matendo mema kwa matumizi yaliyo lazima, illi wasiwe hawana matunda.