Titus 3:5 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
alituokoa si kwa sababu ya jambo lolote jema tulilotenda sisi, bali kwa sababu ya huruma yake, kwa njia ya Roho Mtakatifu anayetujalia tuzaliwe upya na kuwa na maisha mapya kwa kutuosha kwa maji.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
alituokoa, si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyotenda, bali kwa sababu ya rehema zake. Alituokoa kwa kutuosha kwa kuzaliwa mara ya pili na kwa kufanywa wapya kupitia kwa Roho Mtakatifu wa Mungu,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi; bali kwa rehema yake, kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Alituokoa kwa sababu yeye ni mwenye rehema, siyo kwa sababu ya matendo ya haki tuliyotenda na kupata kibali chake, bali ni kwa rehema yake. Yeye aliziosha dhambi zetu, akatupa maisha mapya kwa njia ya Roho Mtakatifu. Ikawa kama kuzaliwa kwa mara ya pili.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
alituokoa. alituokoa si kwa sababu ya jambo lolote jema tulilotenda sisi, bali alituokoa kwa sababu ya huruma yake, kwa njia ya Roho Mtakatifu anayetujalia tuzaliwe upya na kuwa na maisha mapya kwa kutuosha kwa maji.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
alituokoa si kwa sababu ya jambo lolote jema tulilotenda sisi, bali kwa sababu ya huruma yake, kwa njia ya Roho Mtakatifu anayetujalia tuzaliwe upya na kuwa na maisha mapya kwa kutuosha kwa maji.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
alituokoa, si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyotenda, bali kwa sababu ya rehema zake. Alituokoa kwa kutuosha kwa kuzaliwa mara ya pili na kwa kufanywa wapya kwa njia ya Roho Mtakatifu,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
alituokoa, si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyotenda, bali kwa sababu ya rehema zake. Alituokoa kwa kutuosha kwa kuzaliwa mara ya pili na kwa kufanywa wapya kwa njia ya Roho wa Mwenyezi Mungu,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi; bali kwa rehema yake, kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa mara ya pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
alituokoa si kwa sababu ya jambo lolote jema tulilotenda sisi, bali kwa sababu ya huruma yake, kwa njia ya Roho Mtakatifu anayetujalia tuzaliwe upya na kuwa na maisha mapya kwa kutuosha kwa maji.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
akatuokoa sisi, lakini si kwa sababu ya matendo ya wongofu, tuliyofanya sisi; ila kwa huruma yake yeye alituponya akituosha maji ya kutuzaa mara ya pili, tukawa watu wapya kwa kupewa Roho takatifu;
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi; bali kwa rehema yake, kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
alituokoa sisi. Hakufanya vile kwa sababu ya matendo yetu ya haki, lakini alituokoa kwa sababu ya huruma yake kwa njia ya Roho Mutakatifu aliyetuwezesha kuzaliwa mara ya pili na kuwa na maisha mapya kwa kutusafisha kwa maji.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
alituokoa, si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda, bali kwa rehema yake, kwa josho la kuzaliwa kwa pili, na kufanywa upya na Roho Mtakatifu,